Mkakati wa hii kambi kushika nchi 2015 au mapema kabla ya hapo kama wananyotamani si wa kubeza hata kidogo. Ni kikundi hatari sana kinachojivunia ni utajiri haramu waliojikusanyia.mipango yao ni kutibua kazi za serikali ili kufanikisha mikakati yao.
Viongozi walionunuliwa kwa tamaa ya fedha ni wengi sana.miongoni mwao ni mkuu wa taasisi yenye jukumu la kusimamia serikali kwani aligawa nafasi ya uenyeviti wa kamati kwa mstaafu na wafuasi wake.
Nimeshangaa sana hata majuzi kwenye mkutano wa baraza la vijana wajumbe wamepokea "rushwa" ya 50000 kutoka kwa wakala mmoja wapo wa mstaafu huyu.
Wameenda mbali zaidi kwa kumuwezesha mjumbe wao kutoka mkoa wa asali kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuleta mabadiliko ndani ya jumuiya.hii ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu maralia.
KITENDO CHA JK KUWAONYESHA BAADHI YA WATOTO WAKE NDANI YA CCM 'HATI YA URITHI' NDIO HASA IMEGEUKA 'SUMU YA MAMBA' UPENUNI MWAO HIVI SASA
Kama hela ingalikuwa ni kila kitu kiasi hicho basi matajiri wafu wote wangejirejeshea uhai mara moja tu na kujiwekea uzio mkubwa sana kifo kisiwakute hata siku moja duniani.
Mbali na ukweli kwamba hicho kiringe cha kujongea sebuleni kushinwa hata kabla ya safari yake ndefu kufikia malengo dhalimu kuanza, tathmini yangu ni kwamba hakuna mtu amabaye yuko kwenye HATARI KUBWA na kikundi hicho kama Kikwete hapa nchini.
Nasema hivyo kwa misingi ya maelekezo ya fikra kwamba tayari kundi hili, kama toto tundu alivyo kwa mzazi, alishapekua mikabati ya siasa za CCM nchini na kugundua kwamba KWENYE HATI YA URITHI jina kaandikwa yeye kuwa ndiye chanda chema kwa JK kutua uongozi wa Jamhuri ya Muungano wetu huu wa Tanzania.
Lakini kwa kuwa ni wazi kwao kwamba wale watoto wengine ambao majina yao hayamo kwenye hati ya urithi kupewa hata uongozi wa kata lakini wazidi sana tu kupendwa na wana-ukoo wa CCM waliowengi na kusemwasemwa kufaa kwao kumrithi baba yao 2015 basi wasiwasi wote kwa hiki kikundi cha mteule wa urithi waweza kabisa kukituma kufikiria kuhakikisha kwamba Baba 'ANAPISHA' ili uhakika wa urithi huo kutwaa salama mikononi mwao, kwa gharama yoyote ile, inajipa.
Kwa kuhitimisha wazo nawaasa wazazi mnaoandika HATI YA URITHI ndani ya familia zenu, kitendo cha kukiacha ovyo tu ikazagaa tu na kufikika na ama watakaoneemeka na au watakaokosa kabisa 'mgao wa mkate wa familia', kwa tathmini yangu ni jambo la hatari mwisho wa reli Chigoma na hata kuweza kuwa chanzo cha mzazi kupatiwa usafiri wa mapema zaidi ahera na ule uzao wake mwenyewe.
Sumu ya mama ya CCM iko upenuni mwa sebule yao na hivi sasa ina hali ni tete zaidi chini ya bahari na kutiwa wazimu hasa kukikumbukwa KIASI CHA RASILMALI zilizokwishawekeshwa na kikundi chenyewe ndani ya takriban miaka saba mpaka hivi sasa ili wakafikie kwenye ndoto zao hizi za ki-Alinacha Tanzania.