Kambi ya uvuvi ya Migogo yateketea kwa moto, 100 wakosa makazi

Kambi ya uvuvi ya Migogo yateketea kwa moto, 100 wakosa makazi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Zaidi ya watu 100 wamekosa makazi baada moto kuteketeza baadhi ya makazi ya wakazi wa kambi ya uvuvi ya Migogo iliyoko kata ya Maisome Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa Mwanza kuteketea kwa moto muda huu na chanzo cha moto huo bado hakija fahamika.

Ofisa mtendaji Kata ya Maisome, Onesmo Daudi amethibitisha kutokea kwa tukio na hadi sasa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa bado wanafuatia.

Daudi amesema kuwa moto huo umetokea majira ya saa tisa mchana na umeteketeza kabisa baadhi ya makazi ya wakazi wa kambi hiyo.

Kambi ya uvuvi ya Migogo nimiongoni mwa kambi nane za uvuvi wa samaki aina ya sangara na dagaa zilizoko kisiwa cha Maisome wilayani humo.

1615310754765.png
 
Masahihisho ni migongo sio migogo,Niko maeneo ya tukio chanzo cha moto ni mtu aliyekuwa anapima petroleum karibu na moto hivyo kupekekea mlipuko mkubwa sana,mpaka sasa kuna kifo kimoja.

Hasara ya Mali ni kubwa sana haimithiriki
 
Serikali haikutuma janga hilo,wasitegemee chochote.
 
Masahihisho ni migongo sio migogo,Niko maeneo ya tukio chanzo cha moto ni mtu aliyekuwa anapima petroleum karibu na moto hivyo kupekekea mlipuko mkubwa sana,mpaka sasa kuna kifo kimoja.

Hasara ya Mali ni kubwa sana haimithiriki
Aisee kumbe ni mvuvi ?!. Anyway pole yao. Nawajuwa watu wa migongo [emoji120][emoji40]
 
Nipo eneo la tukio, hadi mida ya jioni nimethibitisha kuona mwili wa mbebaji wa mizigo (Mussa) ukiwa umeteketea, hata hivyo kwenye kaya ya bwana aliyejulikana kwa jina la baunsa ambaye alikuwa akiuza petroli amekimbia au atakuwa ameteketea kwa moto.
 
Hizi huwa nimishe za kawaida tu kwenye uvuvi. Sema tu sisi haturipoti sisi siyo watu wa kulialia kama wanafunzi.
 
Eti kambi ya uvuvi ! hawa wavuvi hawana kwao ?
Kamanda kambi ni jina tu, lakini hizi ni sehemu za utafutaji tupo tuliotoka Dar na mikoa tofauti tofauti, kwa taarifa yako wengi wa watu wa huku wanachuma mapesa na wamewekeza mijini na uchangia kiasi kikubwa cha kodi, mafukara ni wachache sana.Hata huyo tajiri mkubwa jijini Mwanza mtiriko wake umeanzia huku.
 
Masahihisho ni migongo sio migogo,Niko maeneo ya tukio chanzo cha moto ni mtu aliyekuwa anapima petroleum karibu na moto hivyo kupekekea mlipuko mkubwa sana,mpaka sasa kuna kifo kimoja.

Hasara ya Mali ni kubwa sana haimithiriki
Hao watu 100 kilammoja angechota maji toka ziwani kwenye ndoo ya Lita 10 wangeweza kuuzima moto huo, hata hivyo ubinafsi chanzo cha nyumba zote hizo kuungua. Wakati moto unaanza na kuona utawashinda nguvu wangeamua kubomoa baadhi ya nyumba ili moto ukose njia, lakini inaonekana hakuna aliyekuwa tayari, hivyo wakaamua kukimbizana na moto wakisahau moto unasaidiwa na upepo uliopo ziwani.
Swali la kizushi, vipi kuhusu samaki hakuna walioungua?
 
Back
Top Bottom