KAMBI YA WAZIRI AWESO MWANZA, HUDUMA MAJI SAFI YAREJEA AWAONYA WATUMISHI
Kambi iliyowekwa jijini Mwanza na Wazir wa maji Jumaa Aweso, imeleta manufaa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya huduma ya maji safi kurejea katika maeneo mbalimbali.
Baada ya kambi hiyo ya siku nne Jiji Mwanza akizunguka maeneo mbalimbali na kukagua miradi mikubwa ya maji na kuzungumza na wananchi huduma ya maji imerejea.
Waziri Aweso ameeleza msimamo huo wa Serikali Jijini Mwanza, baada ya kutembelea na kujiridhisha na tenki kubwa la maji, lenye uwezo wa kubeba lita za ujazo milioni tatu.
Kwa sasa tenki hilo limesheheni maji, hatua iliyosaidia kurejea huduma hiyo katika maeneo ya Buswelu na vitongoji vyake.
Soma Pia: Waziri Jumaa Aweso amsimamisha kazi Meneja wa Usambazaji wa MWAUWASA kwa kushindwa kutekeleza majukumu
Awali tenki hilo lilikuwa halijajazwa maji ambapo baada ya Waziri Aweso kuweka mkazo na kukesha eneo hilo hatimaye limejazwa na wananchi wanaendelea kupata haki yao ya msingi.
Waziri Aweso, pia amesema hatakuwa tayari kumvumilia mtumishi yeyote wa Wizara hiyo, atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kusababisha ukosefu wa huduma za maji nchini.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amir Mkalipa, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya maji, kwa kuwa Serikali inatumia gharama kubwa kwa utekelezaji wake.
Waziri Aweso amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mwanza, ambayo ilikuwa ni maelekezo ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, yenye lengo la kutatua kero ya maji mkoani humo.