KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Kwa sisi raia wa kawaida tumewekewa sheria kuwa haturuhusiwi kupiga picha kambi ya jeshi zaidi zile zenye taarifa muhimu za jeshi. Ndio sipingi na ni sahihi maana kwa kutumia picha tu adui anaweza kupata taarifa nyingi na ikawa ni angamizo kubwa.
Hivi sasa tupo kwenye ulimwengu wa teknolojia tena inakuwa kwa kasi sana,majeshi mengi hivi sasa yanajiimarisha pia katika nyanja hiyo.
Hoja yangu kuu ni kichwa cha habari hapo juu kwani tumekuwa tukizuiwa kupiga picha ama video katika kambi za jeshi,Sasa je vipi satellite ambazo zipo huko juu na huchukua picha nyingi tu na kwa upana zaidi!
Vipi kambi zetu zinajua hilo na wanalizuia vipi wasipigwe picha na satelite?
Ama tunatwanga maji kwenye kinu..?