KIKAO cha Kamisheni ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Geita kimeridhia majimbo mawili ya uchaguzi ya Chato na Busanda yagawanywe kupata majimbo manne ili kuchagiza maendeleo.
Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Mkoa wa Geita, Deodatus Kayango amewasilisha mapendekezo ya mkoa na kisha kuridhiwa na wajumbe wa kikao cha RCC kilichoketi maalum kwa ajili ya kujadili ajenda hiyo.