PreGE2025 Kamisheni ya Ushauri ya Mkoa wa Geita yapitisha mgawanyo wa Majimbo ya Chato na Busanda kwa maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
KIKAO cha Kamisheni ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Geita kimeridhia majimbo mawili ya uchaguzi ya Chato na Busanda yagawanywe kupata majimbo manne ili kuchagiza maendeleo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Mkoa wa Geita, Deodatus Kayango amewasilisha mapendekezo ya mkoa na kisha kuridhiwa na wajumbe wa kikao cha RCC kilichoketi maalum kwa ajili ya kujadili ajenda hiyo.
 
Kikao cha Kamisheni ya Ushauri cha Mkoa wa Geita (RCC),kimeridhia kugawanywa Majimbo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Jimbo la Chato na Jimbo la Busanda ili kupata majimbo manne katika kuchagiza Maendeleo ya Mkoa.

1742054744866.jpeg
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu, Deodatus Kayango wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mkoa na kisha Wajumbe kuridhia katika kikao hicho cha RCC kilichoketi kwa shughuli maalum ya kujadili agenda hiyo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kayango amesema mkoa wa Geita umependekezwa jimbo la Busanda ligawanywe kupata jimbo la Busanda na Jimbo la Butundwe (Katoro) huku jimbo la Chato likigawanywa ili kupata jimbo la Chato Kusini na Chato Kaskazini.

1742054823393.jpeg
Aidha amesema mapendekezo hayo ambayo yatatumwa kwenda Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) yamezingatia vigezo vyote vinavyohitajika pamoja na taarifa rasmi kutoka kwenye vikao vya Halmashauri husika.

Amesema kwenye Wilaya za Mbogwe na Bukombe hakukuwa na mapendekezo ya majimbo mapya huku wilaya ya Nyang’hwale ilikuwa na mapendekezo ya jimbo jipya la Kharumwa na Nyang’hwale yenyewe.

“Katika kigezo cha idadi ya watu, mjini wanatakiwa watu Laki sita na vijijini watu laki nne, kwa jimbo la Busanda ilionekana kuna watu 671,761 na ni kijijini hivyo, tumeona limekidhi vigezo vya kugawanywa, “ amesema Kayango.

“Chato kuna idadi ya watu wapatao 584,963 kwa hiyo na wenyewe wamekidhi vigezo kwenye kigezo hicho tunaweza kupata jimbo la Chato Kaskazini na Chato Kusini, “ amesema Kayango.

“Jimbo la Nyanghwale kuna takribani watu 225,000 na kwa kigezo hicho inaonekana kabisa wazi kwamba haijakidhi vigezo vilivyowasilishwa”, amesema Kayango.” Amesema Kayango.

1742054882987.jpeg
 
Chato ina watu laki 584 lakini chadema walikuwa wanapinga wasijengewe hospitali wala stendi nzuri . Hovyo kabisa
 
Mkuu ni Kamati ya Ushauri ya Mkoa kiingereza
Regional Consultative Committee (RCC) na sio Kamisheni ya Ushauri cha Mkoa wa Geita (RCC)
 
Kikao cha Kamisheni ya Ushauri cha Mkoa wa Geita (RCC),kimeridhia kugawanywa Majimbo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Jimbo la Chato na Jimbo la Busanda ili kupata majimbo manne katika kuchagiza Maendeleo ya Mkoa.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu, Deodatus Kayango wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mkoa na kisha Wajumbe kuridhia katika kikao hicho cha RCC kilichoketi kwa shughuli maalum ya kujadili agenda hiyo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kayango amesema mkoa wa Geita umependekezwa jimbo la Busanda ligawanywe kupata jimbo la Busanda na Jimbo la Butundwe (Katoro) huku jimbo la Chato likigawanywa ili kupata jimbo la Chato Kusini na Chato Kaskazini.

Aidha amesema mapendekezo hayo ambayo yatatumwa kwenda Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) yamezingatia vigezo vyote vinavyohitajika pamoja na taarifa rasmi kutoka kwenye vikao vya Halmashauri husika.

Amesema kwenye Wilaya za Mbogwe na Bukombe hakukuwa na mapendekezo ya majimbo mapya huku wilaya ya Nyang’hwale ilikuwa na mapendekezo ya jimbo jipya la Kharumwa na Nyang’hwale yenyewe.

“Katika kigezo cha idadi ya watu, mjini wanatakiwa watu Laki sita na vijijini watu laki nne, kwa jimbo la Busanda ilionekana kuna watu 671,761 na ni kijijini hivyo, tumeona limekidhi vigezo vya kugawanywa, “ amesema Kayango.

“Chato kuna idadi ya watu wapatao 584,963 kwa hiyo na wenyewe wamekidhi vigezo kwenye kigezo hicho tunaweza kupata jimbo la Chato Kaskazini na Chato Kusini, “ amesema Kayango.

“Jimbo la Nyanghwale kuna takribani watu 225,000 na kwa kigezo hicho inaonekana kabisa wazi kwamba haijakidhi vigezo vilivyowasilishwa”, amesema Kayango.” Amesema Kayango.

Hasara tu, badala ya kupunguza majimbo na posho za wanasiasa ili pesa hizo zilete maendeleo yanayoonekana kwenye jamii !
 
Huku Dar mbona siwasikii??
Kuna jimbo la kawe
 
Zanzibar jambo lina watu 2500 ila mara jambo zima lina watu 500,000
 
Chato hapana, japo Kalemani ameona dalili za kupigwa chini, anatafuta pa kukimbilia
 
Back
Top Bottom