Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

 
Kingai kapandishwa cheo,anakuwa DCI!this is like tap on shoulder!mama anatumia the same script aliyotumia mwendazake,anayechukiwa,ndio unampa cheo zaidi,kama alivyokuwa makonda kwa JPM,sasa huyu mwamba aliyekuwa anaandaa kesi za mchongo Ili kufunga wapinzani,leo anakuwa bosi wa idara ya kuchunguza kesi,"mwenye sumu kaingia hotelini kula,akaambiwa na mwenye hotel,njoo uwe mpishi kabisa jikoni"walaji hawapo salama.
 
Kingai kaulaa Naona IGP katoka kanda pendwa tena!

soon tutasikia wakili Robert kidando yule alikua kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali kwenye kesi ya mbowe nae kateuliwa kuwa jaji.
Rais yoyote mwenye Akili Timamu ni lazima tu atateua Watu wa kutoka Kanda Maalum ( Kwetu Mkoani Mara ) kushika hizi Nafasi za Taasisi Nyeti na za Kimedani.

Kiulinzi na Kiusalama nchi ikiwa chini ya wana Medani wa Mkoani Mara ( Musoma ) itakuwa salama muda wote na Wananchi watafurahi.

Hongera yako sana Poti wangu wa Kikurya na Kizanaki IGP Wambura ila usiache tu mara moja moja kuja Kijiweni Mbezi Beach kwa Mzee Juma ( Mpwae Mzee Nimrod Mkono) kula Nyama na kupiga nasi Stori Nduguzo Wazanaki.

Pia usiache kwenda kuwatembelea Wazee wako unaowaheshimu na Kuwapenda kutokana na Utendaji wao mkubwa na Uliotukuka wenye Uzalendo kwa Taifa hili Wazanaki Wawili akina Mzee Butiku pale Kwake Mabwepande na yule Mwingine ( namhifadhi ) aishiye Jirani na Coco Beach ambao ndiyo walikuwa Mwalimu Nyerere's Think Tanks na bado wanaendelea kutumika Kiushauri mpaka sasa.

Wana Mara ( Musoma ) tunakuombea Majukumu mapya mema, Usiogope, Usitishwe, Jiamini, usimuangushe Rais Samia na mtangulize mno Mwenyezi Mungu kwani najua kuanzia sasa idadi ya Maadui zako itaongezeka.

Mengine nitaongea nawe Inbox Oky?
 
Sirro karudishwa Zimbabwe, akaungane na Roma, Hii ndiyo Tanzania nchi yenye manabii
 
Kingai DCI???AMA SIKUANGAKIA VIZURI
Kweli mkuu labda Nami sijaangalia vema!,huyu mh.hawezi hata kuandika simple statement au to secure crime scene ni zero leo hii ni DCI?lini kama nchi tulichukua wrong turn?,badala ya kuangalia alama ya kutuongoza kwenda mbele, our driver akaaona ni alama ya turn left na matokeo yake tumepotea
 
Yaani mtu anatolewa U IGP anapewa ubalozi, hata kupumzika hakuna. Kingai naona ulisuka vizuri kesi ya Mbowe wakubwa wamekuona. Nchi hii ngoja yaanze ya Sri lanka shenzi type.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…