Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Kingai kaulaa Naona IGP katoka kanda pendwa tena!

soon tutasikia wakili Robert kidando yule alikua kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali kwenye kesi ya mbowe nae kateuliwa kuwa jaji.
Mkurya mwenzangu nasisi tunaendelea kushukuru
 
Ni walewale wa kila siku kubadirishwa vitengo tu. Kwa Siro hana cha kujutia kwasababu wapo waliotoka kwenye kuwa IGP na ubalozi hawakuuonja asirani..
Kama yupi anbaye hakustaafishwa kama yeye?
 
Ubalozi ni cheo kikubwa sana, tena sana, afu 90% ya mabalozi ni Askari, ni vyeo hasa vya kijeshi, pia 80% ya watumishi wa balozi zetu ni TISS.

Ukiwa balozi unakuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, na ukiwa IGP unakuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Balozi anaonekana mdogo kwenu kwakuwa mnahisi Msafara mkubwa ndio ukubwa wa mtu fulani.
Hyo ni demo tu, we ubaloz unaenda kuongoza au kusimamia WaTu wangap??
 
Vigogo Serikalini wanabadilishiwa tu namna ya kula hata kama wanavurunda..anatolewa hapa anapelekwa pale..anatenguliwa na huyu anateuliwa na yule..
Ingependeza sana kama zingekua sinaingia na sura mpya kwenye ngazi za juu ili kuleta mabadiliko. Hizi sura za zamani matokeo yake kujuana kunakua kwingi, flani akikamatwa hakai kituoni hata dak 5 ameachiwa. Ni upumbavu
 
Ubalozi ni cheo kikubwa sana, tena sana, afu 90% ya mabalozi ni Askari, ni vyeo hasa vya kijeshi, pia 80% ya watumishi wa balozi zetu ni TISS.

Ukiwa balozi unakuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, na ukiwa IGP unakuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Balozi anaonekana mdogo kwenu kwakuwa mnahisi Msafara mkubwa ndio ukubwa wa mtu fulani.
Sawa ila katika yeye ni demotion tusidanganyane
 
Zaman hiz za magu na samia cjui Kwanini imekuwa shida IGP kumaliza Muda wake.tatizo jingne jeshi letu linatumiwa sana kisiasa. Na lipo kwenye spot light Sana kuliko majeshi mengine.
Itakuwa hivyo mpk politics itakavokuwa mbali na jeshi hilo
 
Hizo nafasi ni za Kanda maalum kikatiba 😀
Siyo kweli mkuu..
IGP wote kabla ya Sirro hawakutokea huko unakoita Kanda Maalum:
1964-1970: Elangwa N.Shaidi
1970-1973: Hamza Azizi
1973-1975: Samwel H. Pundugu

1975-1980: Philemon N. Mgaya
1980-1984: Solomon Liani

1984-1996: Harun G Mahundi
1996-2006:
Omary Mahita
2006-2013: Saidi A Mwema
2014-2017: Ernest Mangu
2017-2022: Simon Sirro
2022--: Camillius Wambura
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi.

Aliyekuwa IGP Simon Sirro ateulikuwa kuwa balozi nchi Zimbambwe.

Wakati huo huo amefanya mabadiliko ya Makamanda wengine kama inavyoonesha hapa chini
[emoji116][emoji116]

View attachment 2297191View attachment 2297189

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Amemteua Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.

Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: -

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;

Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Hi nchi ya ovyo sanaaa!yaani KINGAI na madudu yote yale kesi ya Mbowe kapewa UDCI??Tutafika mbinguni tumechoka sanaa
 
Back
Top Bottom