Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Teuzi zina mambo yake..chamsingi tunataka katiba mpya mana wateuliwa wote ni walambishwa asali..hawafanyi kwaajili ya watanzania bali kaajili ya aliye wateua.

Waanze kufanyiwa interview mbele ya majaji kisha majina yapeleke bungeni yapigiwe kura...atakayeshinda ndio awe igp.

Tofauti na hapo hao ni watumwa wa aliye wateua.

#MaendeleoHayanaChama
Yan hata iwaje ila katiba haiwezi ruhusu et IGP sijui CDF wapigiwe kura hata siku moja achilia mbali hio interview unayosema haitakuwepo daimaaa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hongera Wambura
Kuchapa kazi kunalipa.

Ninamkubali alipokuwa kinondoni kabla kuhamishwa majambazi yalinyooka na kushika adabu

Hata mama Samia aliwahi.muongelea kama akilalamika uhamisho wake.akihutubia .Ali sent message sijui kama wasikilizaji wahusika walielewa ile meseji.

Kifupi majambazi nchi nzima yajiandae
Wambura ndio.eneo lake analolipenda yatakiona cha mtema kuni.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi.

Aliyekuwa IGP Simon Sirro ateulikuwa kuwa balozi nchi Zimbambwe.

Wakati huo huo amefanya mabadiliko ya Makamanda wengine kama inavyoonesha hapa chini
[emoji116][emoji116]

View attachment 2297191View attachment 2297189

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Amemteua Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.

Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: -

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;

Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Maridhiano ilikuwa ni lazima Sirro aondoke kwanza
 
Katiba mpya itasimamia vema jeshi la polisi lisiumize raia kwa kufuata maagizo ya wanasiasa kama ilivyo Sasa!!hata akiteuliwa yeyote kwenye nafasi yoyote atasimamiwa na Katiba na kutovuka mstari uliochorwa na sheria mama!

Ndio maana sisi wenye hekima tunaimba wimbo huu hapa:-

""Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi.

Aliyekuwa IGP Simon Sirro ateulikuwa kuwa balozi nchi Zimbambwe.

Wakati huo huo amefanya mabadiliko ya Makamanda wengine kama inavyoonesha hapa chini
[emoji116][emoji116]

View attachment 2297191View attachment 2297189

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Amemteua Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.

Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: -

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;

Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Sirro aende na gunia la kubebea pesa Zimbabwe
 
Back
Top Bottom