DOKEZO Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna P. Makakala kuna wahamiaji haramu kutoka China kwenye Wilaya ya Chunya, Kata ya Matundasi, Kijiji cha Itumbi

DOKEZO Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna P. Makakala kuna wahamiaji haramu kutoka China kwenye Wilaya ya Chunya, Kata ya Matundasi, Kijiji cha Itumbi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania ondoka ofisini, na fanya ziara za kiwilaya na kimikoa, nenda katembelee wilaya ya Chunya, Kata ya Matundasi, Kijiji cha Itumbi, kuna wahamiaji haramu kutokea nchini China.

Ukifika hutauliza utajionea mwenyewe. Watu kutokea nchi hiyo ni wengi kupitiliza huko Kijiji cha Itumbi. Wanafanya shughuli gani huko Tumbi utaambiwa.

Wana vibali vya kufanya kazi gani huko utaambiwa.

Je, kazi wanazozifanya huko watanzania wanaweza hadi wakachukuliwe wafanyakazi China utaambiwa?

Wanaishi wapi na kwenye nyumba zipi utaaambiwa

Ofisi ya uhamiaji Wilaya ya Chunya ipo au haipo utaambiwa.

Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Mbeya ipo au haipo utaambiwa.

Ukweli ni kwamba kuna Kila dalili Kamishna Jenerali wa uhamiaji kazi imemshinda au hajui wajibu wake, na chunya kwa ujumla imejaa wakimbizi walio wengi wakitokea china.

Ofisi ya jengo la uhamiaji chunya ni aibu na haistahili, kuwepo tena kwenye wilaya yenye kipato kikubwa kama Chunya, na wilaya yenye wakimbizi na wahamiaji haramu kama Chunya.

Ukifuatilia, idara hiyo nyeti imepewa mtu ambaye hafuatilii na matokeo yake nchi inapoteza mapato, kwa wachina kufanya kazi nchini bila vibali.

Tufike mahali tukubaliane na kauli ya CDF.
 
Back
Top Bottom