Ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa askari wanawake na wasimamizi wa sheria duniani yanayoendelea Chicago nchini Marekani, Kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Tanzania, Suzan Kaganda ametoa mada kuhusu masuala ya polisi jamii na namna ya kushirikisha wananchi, jana Jumanne Septemba 3, 2024.
Pia, Kaganda ametoa uzoefu wake katika masuala ya ulindaji wa amani hususan katika maeneo aliyohudumu ikiwamo kuwa Mkuu wa Operesheni Abyei, Sudan kusini.
CP Suzan Kaganda ametoa uzoefu huo mbele ya washiriki kutoka nchi 64 zilizohudhuria mkutano huo.
“Suala la amani ni jambo ambalo linatakiwa kushirikisha jamii ili amani na utulivu wa eneo husika kuimarika kutokana na ushiriki kamili wa wananchi katika ulinzi wa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi kwani suala la amani ya eneo husika linatakiwa kuanza na jamii husika,”amesema Kaganda.