Kamishna wa ardhi mkoa wa Geita ni mfano wa kuigwa

Kamishna wa ardhi mkoa wa Geita ni mfano wa kuigwa

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Ni vema kusema ukweli. Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Geita ni mfano wa kuigwa. Wananchi wengi wa Mkoa wa Geita wamekuwa wakifuatilia HATI zao kwa muda mrefu bila mafanikio. Kila ukienda unaambiwa njoo kesho, tunaishughulikia, faili halionekani n.k.

Kamishna mwenyewe alifunga safari mwenyewe kwenda ofisi za Ardhi na madudu aliyokutana nayo yanatisha. Baada ya safari hiyo wananchi wengi mfano mimi nimeweza kupata Hati yangu kitu ambacho nimepigwa danadana kwa muda wa miaka mitatu. Mhe. Waziri wa Ardhi na Makazi huyu mtumishi anafaa apewe tuzo na amesaidia sana wananchi wa Geita kupata Hati zao.
 
Back
Top Bottom