Kamishna wa Tume ya Uchaguzi ajiuzulu, asema tume imegawanyika na inafanya kazi bila kuzingatia utaratibu

Kwenye mambo ya chaguzi tuna nafuu gani?!
Wewe ndiyo useme ni maeneo gani hapa Tanzania ambayo unaona kina tatizo ili tukujibu, ukiuliza swali la wazi kama hili, utapata jibu la wazi, kwamba tuna nafuu katika maeneo yote ya uchaguzi
 
The lady was afraid of being "Msandoed" labda...Her brother and family alledgedly left the country after being threatened...I also think she wanted to keep her international professional career alive...
 
Wewe ndiyo useme ni maeneo gani hapa Tanzania ambayo unaona kina tatizo ili tukujibu, ukiuliza swali la wazi kama hili, utapata jibu la wazi, kwamba tuna nafuu katika maeneo yote ya uchaguzi
Kama huna ushabiki basi jadili jambo hili kwa swala la haki
Uchaguzi unasimamiwa na wakurugenzi wa halmashauri za miji na wilaya, akishirikiana na watumishi walio chini yake, ambao wote ni wateule na wanufafaika wa mh. Rais aliyepo!! Na wakati huo, Rais na na Chama chake ni washiriki wa chaguzi hizo dhidi ya vyama na wagombea wengine!!! HAPA KUNA HAKI GANI KWA WAGOMBEA WENGINE?!

Lakini pili sheria zetu za uchaguzi si nzuri, zinategemea zaidi busara kuliko haki. Mfano hii ya mtu ngazi ya urais, akishatangazwa hata kama ni kwa shinikizo kutoka popote, hauwezi kuhoji popote!!! KATIKA KARNE HII???

Mambo ni mengi sana, tulibadili katiba kidogo, ili kuingia mfumo wa vyama vingi lakini sheria zetu zilibaki kuwa za mfumo wa Chama kimoja!! Na hili liko wazi
 
Sasa kipi kati ya hayo uliyo yataja ni kinyume na sheria au katiba yetu tuliyo kubaliana?
Tanzania hatuna matata....ukitaka yabadilike unajua taratibu za kufata...
 
Kwanza ninaomba tuelewane, kuna haki na sheria, hivi ni vitu viwili tofauti, ila sheria zinawekwa ili kutoa haki. Tanzania inaongozwa na sheria mama ambayo ni katiba ya mwaka 1977, lazima uchaguzi usimamiwe na uendeshwe kwa mujibu wa sheria zetu tulizojiwekea, na tunafanya hivyo, hao wote uliowataja, wakurugenzi, rais na wengine, wote hao wamepewa madaraka hayo kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hakuna kitu kilichokeukwa, hoja yako unaona sio haki kwa wao kusimamia kwa sababu ni wanufaika wa rais ambaye na yeye ni mgombea, hilo siwezi kukukatalia moja kwa moja, lakini hilo lipo karibu nchi zote, kwa mfano, sasa hivi Uhuru ni mgombea wa urais, lakini katiba inamruhusu kukutana na wawakilishi kutoka county mbalimbali pale Ikulu ya Kenya, je hiyo ni haki?, bado ana mamlaka ya kutumia vyombo vya dola kuzuia maandamano ya wapinzani, je hiyo ni haki?, bado ana mamlaka ya kupitisha na kusaini sheria kandamizi za uchaguzi, je hiyo ni haki?, sasa ukiondoa hilo la kupinga matokeo mahakamani, nini zaidi walichotuzidi?
 
Sasa kipi kati ya hayo uliyo yataja ni kinyume na sheria au katiba yetu tuliyo kubaliana?
Tanzania hatuna matata....ukitaka yabadilike unajua taratibu za kufata...
Unakimbilia kudai mlikubaliana na nani?! Yaani katiba ya msekwa unadai mlikubalia na na nani?! Nilidhani hauna ushabiki kumbe walewale!! Najuta
 
Ruttashobolwa niliposema tuliifanyia marekebisho katiba yetu, kuruhusu multi party democracy, hatukurekebisha na sheria zetu kufanya chaguzi zetu kuwa za huru na haki. Mwanya ulikuwapo kwenye Bunge la katiba lakini unafki wa Kikwete na marehemu Sitta umeturudisha nyuma zaidi!!! Na hili kilichowasumbua ni maslahi ya Chama na si taifa!! Pole yetu
 
Bado unatoa maoni ambayo sio yoteunayosema ni kweli au ni sawa, unapotoa maoni ni muhimu kuwa na taarifa sahihi kwa lile unalolisema, Kikwete hajafanya kosa lolote katika mchakato mzima wa katiba, kinachojitokeza kwako, wewe ni mkereketwa zaidi badala ya kuwa mchambuzi wa kisiasa, ukishaingiza ukereketwa unakosa umakini katika kufanfanya uchambuzi wa kina, hebu niambie tatizo gani wewe unaloliona katika mchakato mzima wa kuipata katiba mpya hadi umlaumu Kikwete?
 
Reactions: Oii
October 18, 2017 patrick


Kiongozi wa juu wa Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) amejiuzuru, akisema kuwa nchi yake haitaweza kuandaa uchaguzi huru na haki unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Roselyn Akombe, amesema, IEBC imekuwa kwenye “kizungumkuti”, cha siasa nchini humo, na hivyo kushindwa kufikia makubaliano au uamuzi wowote.

Akiwa nchini Marekani anakofanyia kazi, ameiambia BBC kuwa, amekuwa na hofu na maisha yake alipokuwa nchini Kenya, baada ya kupokea vitisho vingi.

Juma lililopita, kiongozi wa upinzani, Raila Odinga alijitoa katika uchaguzi wa marudio wa urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26.

Mahakama ya Juu nchini humo, ilifuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, ambao ulimtangaza mshindi Rais wa sasa Uhuru Kenyatta baada ya kukiukwa kwa taratibu.

Katika taarifa yake, Akombe amesema amekuwa na ” wasiwasi juu ya uamuzi wake wa kuondoka IEBC (Independent Electoral and Boundaries Commission).

Na kuongeza ” Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC unaweza kuwavunja moyo baadhi yenu, lakini siyo kwa kukosa kujaribu.

“Nimejaribu kwa kadri ya uwezo wangu kutokana na hali iliyopo. Kuna wakati unatakiwa kuondoka, hususan wakati pale maisha ya watu muhimu yanawekwa rehani. Tume hiyo imekuwa sehemu ya hali tete inayoendelea nchini humo.Tume hiyo imezingirwa.

“Tume hiyo kwa sasa haina uhakika wa kuendesha uchaguzi huru na haki Oktoba 26, 2017.”
 
Huyo ndiye alieivuruga katiba mpya alipoenda kulizindua Bunge hilo. Alipolazimisha Warioba atangulie na kisha yeye atoke nyuma na kupondea rasimu kwa ujumla wake. Na wabunge wa ccm kama unavyowajuwa, hawana usemi juu ya Rais wao, wao ni kuitika ndiyooooo hata kama jambo la kukwamisha taifa. Bahati mbaya kuanzia hapo wajumbe waligawanyika, na kuhakikisha wanakwamisha so here we are!!
 
Humu Lumumba niwengi balaa wazee wakulazimisha maji ya mchele kuwa maziwa.
Lini Tz tukaizidi Kenya?? Kuanzia democracy had uchumi?
Tsh 1000000= Ksh 45000 huoni tofauti hapo? Lumumba punguzeni mahaba katiba ya Tz ni ya msekwa na ccm wala sio katiba ya wananchi
 
Kwani Tanzania kuna wapinzani?? Ama wachumia tumbo!!?? Kumbuka movie ya Chadema na Mhe. Lowassa!!
 
Kikwete kama mwenyekiti wa CCM wakati ule, hakuhitaji kwenda kwenye bunge ili kuwajengea msimamo wabunge wa CCM katika jambo lile, tayari wabunge wote wa CCM walikuwa wameshakubaliana kwamba wapiganie serikali mbili, kwa sababu hiyo ndiyo sera ya chama chao, kusema Kitendo cha Kikwete kwenda na kuhutubia bungeni ndicho kilichofanya wabunge wa CCM wabadili msimamo sio cha kweli na hakina mashiko yoyote, kuhusu Kikwete kumtanguliza Warioba, hilo hata mimi sikulielewa na hadi leo sijapata jibu
 
Uwezo wako ni mdogo sana, ni aibu kujibishana na wewe, endelea kupiga domo.
 
Kama Rais alitakiwa kuwaacha wajumbe huru, lakini alipoonyesha kutofautiana na wajumbe wa kamati aliowatuma yeye kukusanya maoni kwa wananchi, basi angalau angelifanya sirini lakini si hadharani !!
Kuanzia hapo mpasuko umekuwa zaidi kwa wale walioitetea rasimu na wale waliomuunga mkono mwenyekiti wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…