Kwanza ninaomba tuelewane, kuna haki na sheria, hivi ni vitu viwili tofauti, ila sheria zinawekwa ili kutoa haki. Tanzania inaongozwa na sheria mama ambayo ni katiba ya mwaka 1977, lazima uchaguzi usimamiwe na uendeshwe kwa mujibu wa sheria zetu tulizojiwekea, na tunafanya hivyo, hao wote uliowataja, wakurugenzi, rais na wengine, wote hao wamepewa madaraka hayo kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hakuna kitu kilichokeukwa, hoja yako unaona sio haki kwa wao kusimamia kwa sababu ni wanufaika wa rais ambaye na yeye ni mgombea, hilo siwezi kukukatalia moja kwa moja, lakini hilo lipo karibu nchi zote, kwa mfano, sasa hivi Uhuru ni mgombea wa urais, lakini katiba inamruhusu kukutana na wawakilishi kutoka county mbalimbali pale Ikulu ya Kenya, je hiyo ni haki?, bado ana mamlaka ya kutumia vyombo vya dola kuzuia maandamano ya wapinzani, je hiyo ni haki?, bado ana mamlaka ya kupitisha na kusaini sheria kandamizi za uchaguzi, je hiyo ni haki?, sasa ukiondoa hilo la kupinga matokeo mahakamani, nini zaidi walichotuzidi?