Kamishna wa Tume ya Uchaguzi ajiuzulu, asema tume imegawanyika na inafanya kazi bila kuzingatia utaratibu

Hayo unayosema ni maoni yako, mimi sina haki ya kuyapinga, lakini sina uhakika sana kama ni sawa, ila katika nchi ya demokrasia kila mtu ana haki ya kutoa ushauri na msimamo wake katika jambo lolote, akiwemo rais, ila haruhusiwi kuwalazimisha wapiga kura, amelifanya jambo hili Nyerere, Obama amekuwa akilofanya katika Bunge la Senate mara nyingi tu.
 
Africa bhanah na viongozi wake....njaa kali ya madaraka....
 
Rais alikuwa na nafasi yake kabla ya kulifikia bunge la katiba!! Na neno moja watu waelewe si kila takwa la Rais ni jambo zuri. Hebu chukulia suala la gas na mafuta!! Wenzenu walishauri angalau lisubiri huyo mtu astaafu, asilete uharaka!! Lakini walibezwa na kudharaulika na kisha kutimuliwa bungeni!! Leo tunajuta hakuna tofauti na yaliotokea kwenye madini !! Sasa hapo takwa la Rais lilikuwa na maslahi na nchi?! HAPANA RAIS ASIWE KILA KITU
 
Kwanza ninakuomba usirukeruke wakati tinajadili mambo ya msingi kama haya, hakuna mtu yeyote aliyesema wala anayedhani kuwa rais hakosei, kwa kulijua hilo, ndiyo sababu rais kama mwananchi mwengine ana kura moja tu, ila kama rais ana nafasi na haki ya kwenda na kulihutibia bunge wakati wowote ule apendavyo, hiyo ni haki aliyonayo kisheria, wewe unadhani haikuwa wakati mzuri kwa yeye kwenda kuhutubia na kuyasema yale aliyosema pale bungeni siku ile, ninarudia tena, yeye kama rais hajavunja sheria wala kanuni yoyote ya kiuongozi, ametumia haki yake ya kikatiba, na busara zake zilimtuma aseme yale aliyosema, wewe unahisi alikosea, ni haki yako kihisi hivyo kama ambavyo ni haki yake yeye kuhisi yale maneno alipaswa kuyasema, watu wanaweza kutofautiana, lakini muhimu ni kwamba hajavunja sheria ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…