Kamishna wa Uhamiaji Manyara amejibu hoja Kisomi; ni kweli katika macho ya sheria gari na bendera siyo mali ya CCM; CHADEMA kuweni makini na hii move

Kilichojibiwa na Idara ya Uhamiaji ndicho kinachoitwa majibu katika macho ya sheria. Si kila bendera ya kijani ni bendera

Mwanagenzi

Soma Uhamiaji: Dereva na V8 Iliyobeba wahamiaji Haramu 20 wa Ethiopia Isihusishwe na CCM
Na ingekuwa gari ya ccm hao wahalifu wasinge kamatwa tatizo hao na ilo gari walikua wahalifu feki wa ccm na gari feki la ccm .... wakati chama na serikali kinataka wahalifu OG maana vitendo vya kihalifu kama hivyo vinafanywa siku zote na ccm huku polisi wakisimama kwa ukakamavu na kuvipigia saruti ...na kuakikisha yoyote anaye hoji au kuuliza au kupiga picha ana shughulikiwa kikamilifu ....ccm ni mafii ya kuku
 
Viongozi wengine waache kuwa na urafiki wa karibu na madereva kiasi cha kuwaachia magari hovyo
Kuna wengine wanaletewa chicks na kuwafanya wasiri wao
Hata dereva akisema anaenda kwao weekend anamuomba gari

Sasa na wao wanajiongeza kwa magendo
Nimewaza tu kwa sauti maana tunajuana hata matajiri wengi wanawatumia madereva wao kuwaletea mademu
Siku kikisanuka anarukwa maili kumi
 
Maelezo ya aina hii yalipaswa kutolewa na Makonda kama Msemaji wa CCM. Kutolewa na huyo Afisa kunaongeza maswali mengi yanayokosa majibu. Tunatarajia pia, kama maelezo ya Afisa ni ya kweli, CCM kumburuza mahakamani mmiliki wa v8 husika kwa udhalilishaji wa chama chao. Ama sivyo...
 
Nichukue nafasi hii kumpongeza samia kwa uongozi uliotukuka na kuboresha nyanja ya usafirishaji hakika mama anaupiga mwingi sana mitano tena kwa mama
 
Ajibu kisomi au kadiri ya upendavyo,CCM ni kikundi cha watu wengi wahalifu katika nchi hii.Hilo halihitaji utetezi na mbinu wala mbwembwe nyingi za kujikwamua na dhahma.Si mara moja au kumi watu wanaojinasibisha na CCM kutuhumiwa,kuhisiwa,kukutwa,kuthibitika bila shaka kuwa ni wahalifu kwa mgongo wa itikadi za chama chao.Kujitetea sana ni kulazimisha mkondo wa maji uhame bila sababu yenye kueleweka.
 
Abishe na hayo.
 
Hapana. Yeye angezungumzia kuhusu mambo ya uhamiaji. Bendera haimhusu.
 
NINGEPENDA KUJUA NANI MMILIKI WA HIYO GARI?

ova
 
Tafiti zinazoonesha kila msomalia au Ethiopian ,wasudani wakitaka kuvushwa hulipa Dola zisizopungua #5000 kwahiyo walikuwa 20 mwanaccm hakuwa mjinga kutaka kujaribu
Na hiyo ilikuwa arobaini yake imefika huyo ndiyo michezo yake. Watu wanajiunga au kuisapoti CCM ili kupata kivuli cha kufanya maovu yao . CCM ni kusanyiko la watenda maovu
 
Huwezi kukata tawi ulilolikalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…