Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ahoji kuhusu Usalama wa Taarifa zilizokusanywa na Sarafu Mtandao ya 'Worldcoin'

Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ahoji kuhusu Usalama wa Taarifa zilizokusanywa na Sarafu Mtandao ya 'Worldcoin'

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1690994653896.png
Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) na Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Data (ODPC) wameelezea kutoridhishwa kwao kuhusu mradi wa Sarafu Mtandao "Crypto" unaoenezwa na mtandao wa Worldcoin.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo Agosti 2, 2023 na Taasisi mbili za Umma, zimeangazia wasiwasi wa usalama wa Taarifa Binafsi za Wananchi zilizokusanywa siku chache zilizopita tangu kuzinduliwa kwa mradi huo tata ambapo zaidi ya Wakenya 350,000 tayari wamejisajili.

Mkurugenzi Mtendaji wa CA, Ezra Chiloba na Kamishna wa Data (Taarifa Binafsi) Immaculate Kassait walitilia shaka ukosefu wa mfumo na taarifa za kampuni ya Worldcoin na hasa kuhusu usalama wa Taarifa Nyeti zilizokusanywa kutoka kwa Wananchi pamoja na masuala ya usalama mtandaoni yanayohusu mchakato mzima.
1691031861428.png

Pia wamehoji sababu za msingi kwa Wananchi kupewa zawadi ya pesa taslimu Tsh. 120,385 baada ya kusajiliwa, na mtandao huo ambapo wamedokeza kuwa suala hilo lina kila dalili ya ukiukaji wa sheria.

"Tangu kuzinduliwa kwa shughuli za WorldCoin nchini Kenya, Taasisi za CA na ODPC zimefanya mapitio ya awali na kubainisha masuala kadhaa ya kisheria ya udhibiti ambayo yanahitaji uangalizi wa haraka," ilisomeka taarifa hiyo.

"Masuala hayo ni pamoja na kukosekana kwa uwazi juu ya usalama na uhifadhi wa data nyeti iliyokusanywa (Utambuzi wa Sura na Mboni ya Jicho), kupata taarifa binafsi bila kibali cha watumiaji kwa kubadilishana na malipo ya pesa ambayo yanatokana na ushawishi, kutokuwa na uhakika kuhusu ulinzi wa taarifa za watumiaji kwenye Sarafu Mtandao na uhusiano wake. Huduma za ICT, taarifa zisizojitosheleza kuhusu ulinzi na viwango vya usalama mtandaoni na taarifa za raia kuwa mikononi mwa watendaji binafsi bila mfumo unaofaa.”

Pia taasisi hizo zimeongeza kuwa: "Masuala haya yanahitaji uchunguzi wa kina ili kuwezesha wadhibiti kushauri wadau juu ya hatua zinazofaa kulinda masilahi ya umma."

Kwa hivyo, CA na ODPC zinaunga mkono hatua ya serikali ya kusitisha shughuli za Worldcoin, na kuzitaka mamlaka husika kufuatilia kwa makini mradi huo katika jitihada za kuangazia msingi wa huduma zake na kuwalinda Wakenya dhidi ya kukumbwa na ulaghai.

“Kutokana na uchunguzi huu wa awali, uchunguzi wa mashirika mbalimbali unaendelea. Kwa hivyo, na kama ilivyoagizwa na serikali, Worldcoin lazima isitishe shughuli zake za ukusanyaji wa data nchini Kenya hadi ilani nyingine itakapotolewa,” Chiloba na Kassait walibainisha.

Aidha, taasisi hizo zimewatahadharisha Wananchi kuwa waangalifu hasa wanatoa taarifa zao kwa makampuni ya kimataifa, na kusisitiza kwamba baadhi ya nchi za Ulaya pia zimeibua wasiwasi kuhusu Worldcoin.

"Migogoro kuhusu Worldcoin sio mipya. Wasiwasi kama huo umetolewa katika maeneo mengine kama Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na India," walibainisha.

"Umma unashauriwa kuchukua tahadhari wakati wa kutoa taarifa binafsi kwa mashirika au kampuni binfasi"

Kampuni ya Worldcoin imepigwa marufuku kuendelea na shughuli zake nchini Kenya baada Waziri wa Mambo ya Ndani Prof. Kithure Kindiki kwa kile alichokiita "maswala ya usalama wa taifa."

Worldcoin, ambayo inamilikiwa na Sam Altman, mmiliki wa kampuni kutoka Marekani inahusika na masuala ya Akili Unde (AI) ya ChatGPT, ina mchakato wa usajili unaohusisha kuchukua taarifa za utambuzi kutoka kwenye mboni za jicho la mtu ili kubadilishana na utambulisho wa kidijitali unaoitwa World ID.

Wale wanaovutiwa na huduma hiyo hupata tokeni 25 za sarafu za Crypto bila malipo zinazojulikana kama WLD ambazo kwa sasa zina thamani ya Tsh. 141.9858 huku bei ya tokeni moja ikiuzwa kwa Tsh. 5,931.

Pia soma: Je, unaweza kumpa mtu nafasi ya kumiliki utambulisho wako milele kwa gharama ya Ksh. 7,000 (sawa na Tsh. 120,000/-)?
 
Back
Top Bottom