Ndugu Wana JF,
Jana baada ya kutoka safari, jirani yangu alinipigia simu akinieleza kuwa amekorofishana na mke wake na kuamua kuondoka nyumbani mpaka yule mke wake atakapoondoka nyumbani. Aliniomba niangalie ufunguo kama ameuacha yule mke wake kwani alikuwa kamwambia kwamba anaondoka hiyo jana. Nilimuuliza alipo, akasema yupo mitaani na atakuja nieleza akirudi nyumabi. Nilipoangalia ufunguo, niliona kweli umeachwa na mke wake keshatimuka kabisa. Je ni sawa kumkimbia mke wako na kukaa mtaani kusikojulikana, kisa mumekorofishana? Kwa nini asimsafirishe moja kwa moja na kumkabidhi kwao?
Nawakilisha wana JF