Kamkimbia Mke Wake, Kisa Wamekorofishana Na Mpaka Aondoke Nyumbani Ndo Arudi

Kamkimbia Mke Wake, Kisa Wamekorofishana Na Mpaka Aondoke Nyumbani Ndo Arudi

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
1,639
Reaction score
519
Ndugu Wana JF,
Jana baada ya kutoka safari, jirani yangu alinipigia simu akinieleza kuwa amekorofishana na mke wake na kuamua kuondoka nyumbani mpaka yule mke wake atakapoondoka nyumbani. Aliniomba niangalie ufunguo kama ameuacha yule mke wake kwani alikuwa kamwambia kwamba anaondoka hiyo jana. Nilimuuliza alipo, akasema yupo mitaani na atakuja nieleza akirudi nyumabi. Nilipoangalia ufunguo, niliona kweli umeachwa na mke wake keshatimuka kabisa. Je ni sawa kumkimbia mke wako na kukaa mtaani kusikojulikana, kisa mumekorofishana? Kwa nini asimsafirishe moja kwa moja na kumkabidhi kwao?

Nawakilisha wana JF
 
Huo ni udhaifu mkubwa kwa mwanaume japo yawezekana kazidiwa kete
 
Si udhaifu,

Kero zinaweza kukuzidi na ukaona hatua iliyopo ni wewe kuondoka tu !

Wala msikimbilie kusema kuwa kamkimbia, na huwezi kujua ni mara ngapi muhusika maejaribu kutatua hayo matatizo, ametumia mbinu gani? Amepata ushirikianao kiasi gani kwa mwenzie...............amina nakuambia kuna wakati haya matatizo ya kifamilia yanafika mahali hupati msaada wa harakana wengine ndi hujiua ama kudhuru mwenzi; binafsi naona alichokifanya ni busara...................ameondoka!

Sasa rudi kwa rafiki yako ukampe ushauri nasaha na si kum label kuwa kamkimbia mkewe..................hayajakukuta ndio maan wabwatuka namna hii!
 
labda amegundua mkewe ni jini ndo maana hataki hata kumuona anavyoondoka...!!
 
Huyo ni mkewe wa ndoa au ni walichukuana(walibebana)? Kama kweli ni mkewe na bado anampenda kwa nini amkimbie? Kukimbia sio soln ya kumaliza tatizo angekaa wakaongea wakayamaliza
 
mmmh
nadhani alifanya uamuzi mzuri maana huwezi jua matoke ya hasira yake ingekua nini...
angweza kuua au hata kujiua
afadhali alitumia busara
 
Huyo ni mkewe wa ndoa au ni walichukuana(walibebana)? Kama kweli ni mkewe na bado anampenda kwa nini amkimbie? Kukimbia sio soln ya kumaliza tatizo angekaa wakaongea wakayamaliza

Mwanzo kabisa huyu jamaa alinieleza kwamba anauzoefu mkubwa sana na wanawake kwani ameoa kabla na kupata watoto na huyo alikuwa mke wake wa nne. Yeye na mke wake wamebahatika kupata mtoto kama miezia mitano iliyopita. Kwa kweli alimusifia sana huyu mke wake wa mwisho kuwa ni muelewa sana. Yaani hata mimi imenisurprise sana na nafikiri imemchukua muda mrefu kunijulisha kulingana na jinsi alivyokuwa akimsifia huyo mke wake. Sasa sijui tatizo ni nini. Mimi navuta subira ili anijulishe kilichojili.
 
Back
Top Bottom