Kampala International University (KIU) chafungiwa na TCU

Kampala International University (KIU) chafungiwa na TCU

kama huelewi kitu si uulize? sasa mba evening program unadhani ni ya miezi sita!!! agh!!!

Nakwambia hivi,hakuna MBA ya miaka miwili Tanzania,huo mi muda tu ambao unatakiwa uwe umekamilisha course yako,lakini yaweza kuwa chini ya hapo.
 
TCU hongereni kwa hatua hii mliochukua dhidi ya KIU ila napenda kuwaambia ya kwamba bado mna kazi kubwa ya kuondoa ubabaishaji na usanii uliopo katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini lakini tambueni ya kwamba na ninyi ni sehemu ya ubabaishaji unaoendelea katika vyuo vikuu mbalimbali na hili mnalijua. fikeni hadi kwenye vyuo vikuu vilivyopo mikoani mchunguze mambo ya vyuo hivyo.
 
Ni Tawi la Kampala kweli ama kuna mhuni anapiga hela kwa mgongo wa Kampala?
 
kwakweli this government inabidi i take masuala ya elimu seriously..huko tunapokwenda hata sijui watoto wetu watakuja kuwa na maisha gani kwa mfumo huu wa elimu..

nobody cares kila mwenye nafasi anaangalia atafaidika vipi yy kama yy kupitia nafasi aliyonayo.. mh so sad..
Utasikia kina mikono ya mawaziri kwenye hicho chuo.
 
....bora wakifungie...na sitashangaa share holders wenye kumiliki hiki chuo ni vigogo serikalini....Hivi ndio vyuo vilivyoanzishwa kama uyoga ili kubeba ma feki yanayotokana na shule zetu....Chuo kinawezaje kutoa masters/PhD kwa kuwa na waalimu wenye masters tu??..au PhD za kuunga??.....The quality of university education can also be measured by the quality of university itself...but this fact seems to be taken differently by some universities in TZ....this one being among....

Hapa vyuo vingi tu sio hicho tu vinatakiwa viangaliwe pia maana vimeanzishwa kama uyoga na ukifanya tathimini ya kina utagundua though inatoa degree but ukiwafanyia tathimini wanachuo wanaotoka hivyo vyuo utagundua elimu waliyopata ni kama diploma flani maana kuna ambao unawaona wepesi kabisa hata wenye diploma wana afadhali. Tatizo vyuo vingi lipo kwenye wahadhiri ambao nao wamezaklishwa chapchap na wengi wao wana masters ambao pia experience yao katika kazi unakuta ipo limited kutokana na wahadhiri hao wanapelekwa puta kwa elimu ya haraka haraka ili kukidhi mahitaji lakini ukweli unabaki palepale kwamba chuo ili kiwe chuo kinahitaji kuwa na wahadhiri wengi walio kwenye game muda mrefu na wachache wa kizazi kipya wanakuwa wanapanda mdogo mdogo lakini siku hizi mtu ana maliza leo anabakishwa chuo kisa amepata first class baada ya miezi 18 ana masters huku akiendelea kufundisha.

Wangekuwa wanavipandisha hadhi hivi vyuo mdogo mdogo kama vile walivyofanya kwa Mzumbe, Ushirika na vingine ambavyo vimekuwa vikitoa fani mbambali katika diploma level tena wakati wanavipandisha wangeacha viendelee kutoa kozi ambazo zilikuwa zinatolewa na hivyo vyuo ata diploma level huku wakiongeza fani zingine tofauti tofauti sio kama siku hizi chuo kinapandishwa hadhi alafu kinaanza kutoa makozi kibao
 
Chuo kikuu cha Kampala tawi la Tanzania (KIU) kimefungiwa na TCU kutoa mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kwa kutokuwa na sifa stahiki za wahadhiri wa kutoa mafunzo hayo.

TUESDAY, MAY 07, 2013

kama mnakumbuka kuna kipindi uliletwa mtihani wa hiki chuo hapa JF wa somo la computer ambao ulikuwa unasikitisha kweli ulikuwa kule jamii photos

probably TCU walianzia hapa Jf na kuamua kufuatilia!

sasa na we jamaa ukaamini kitu kilichofanyiwa photoshop?? mtu yeyote pia anaweza kutengeneza pepa kama ile ikaonekana ni ya UD ...... hiyo sio sababu
 
Hivi kimefungiwa kwa sababu ni Private au?? Mbona kuna UDOM inadahili wanafunzi wa Masters na PhD bila kuwa na walimu wanaostahili? Kwa UDOM Asst Lecturer ni mtu mkubwa sana. Anafundisha hadi wanafunzi wa PhD. Mwalimu yeyoyte mwenye idea kidogo sana ya somo fulani anaambiwa afundishe. TAs ni walimu wa kutumainiwa sana. Kama kweli TCU wako serious, basi waichunguze UDOM pia. Au wanajua ila wameamua kufumba macho.

TCU wanafanya kama serkali. Ili shule binafsi isajiliwe lazima iwe na maabara, uwanja wa michezo, fence, etc. Lakini za serkali zinafunguliwa hata kabla majengo ya madarasa hayajakamilka. Huu ni uonezi mkubwa. Lkn hii strictness kwa shule za binafsi umezisaidia kwani performance zao ni nzuri sana ukilinganisha na za serkali.
 
Back
Top Bottom