Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Katavi, Thomas Maganga, ametoa wito mzito bungeni akitaka hatua za dharura zichukuliwe kuokoa watoto na kizazi kijacho dhidi ya wimbi la mmomonyoko wa maadili na vitendo vya ushoga. Maganga alionya kuwa hali ni mbaya akisisitiza kuwa ikiwa kizazi cha sasa kimeshindikana, ni lazima nguvu kubwa ielekezwe kulinda watoto wadogo kwa kuingiza mitaala madhubuti ya maadili kuanzia ngazi ya chekechea, shule za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.
Maganga alibainisha kuwa mabadiliko ya tabia yanayoonekana kwa baadhi ya vijana mitaani hivi sasa ni matokeo ya "uwekezaji mchafu" ulioanza zaidi ya miaka 10 iliyopita, hivyo serikali lazima ianze kuwekeza sasa kwenye kinga.
Alizitaka Wizara ya Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kuacha lugha zisizoeleweka na badala yake zitumie mitaala iliyo wazi itakayomfundisha mtoto tangu akiwa mdogo kutambua kuwa kuguswa au kusogelewa katika maeneo yake ya siri ni kosa kubwa.