Uchaguzi 2020 Kampeni bila kukidhi kiu ya walengwa za nini?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Malengo ya kampeni ni kuonyesha kwa nini mgombea mmoja anafaa kuliko mwingine. Kujinadi kwa wapiga kura na hata kupigana madongo kwa wagombea ndiyo sehemu ya mchezo wenyewe.

Wagombea wote ni shuruti wawe katika uwanja sawa ili mwananchi ajichagulie mwenyewe anayemtaka bila ya shinikizo lolote.

Mlaji katika biashara hii ni mwananchi. Mwananchi ana nia ya dhati kabisa ya kujua kwa nini huyu wala siyo yule.

Mamlaka yoyote inapoingilia kati kumbeba mgombea mmoja kwa mbeleko dhidi ya wengine si sawa. Kimsingi ni kuwanyima wananchi kwa makusudi fursa yao ya kuwachagua wenye hoja na wanaowataka.

Tume ya uchaguzi - rudisheni wagombea wote walioenguliwa kwa visababu visivyo na mashiko. Visababu vya kiuhakiki ambapo nyie wenyewe mlikuwa na wajibu wa kuvitolea maelekezo visiendekezwe. Wapeni watu haki zao za kutumia sanduku la kura kufanya maamuzi yao.

Vipi kukiukwa kwa haki za wagombea kutokana na vikwazo mbalimbali visivyo kuwa na vichwa wala miguu tokea mamlaka zingine? Vipi kanuni na lugha za kienyeji kutumika majukwaani? Vipi matumizi ya pesa kununua wasanii na hata wagombea?

Polisi - hadi sasa tukiacha dosari kidogo kidogo mmejitahidi. Yale mambo ya kuwakamata baadhi ya wagombea ili wasirudishe fomu zao kwa wakati hatukuyapenda.

Tunaamini tume itatumia busara kuwarejesha wagombea wote waliokwamishwa na kadhia zisizokuwa na sababu pamoja na hizi za tokea kwa baadhi ya polisi wasiokuwa na kutambua umuhimu wa haki za watu.

Vyombo vya habari - kwa hofu zenu, kununuliwa kwenu, kujipendekeza kwenu nk, mmewanyima wananchi kuwasikia wagombea wakijinadi. Nyie hamna dhamana ya kuwaamulia watu wasikie au wasisikie nini. Si sahihi kwenu kuwanyima watu fursa ya kuwasikia wagombea katika kampeni zao.

Mamlaka zote, TCRA, TCAA, mahakama nk, ni muhimu mno mkajitathimni. Hii kushindana kwa mamlaka kumfurahisha mgombea fulani haitutendei haki sisi wananchi. Historia ni shuhuda mzuri na kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe.

Kwani wagombea hawajui wananchi wanahitaji nini kiasi cha kuingiliwa kwa mchakato huu na mamlaka hizi?

Wagombea wote ni watanzania wenye haki sawa za kukamata uongozi wa juu wa nchi hii. Ubaguzi huu wa nini basi?

Tunahitaji wagombea wakidhi mahitaji yetu ya msingi tunayotarajia kwao. Kama hilo halipo, mengine yanabakia kuwa upuuzi mtupu kama huu wa kulazimishana na ahadi zenye mielekeo ya rushwa zaidi.

Mamlaka na zikatambue, haki na uhuru wetu katika zoezi zima la kampeni ni lazima kuheshimiwa.
 
Maadili ya Nchi ni muhimu sana kuliko mgombea mmoja anayeporomosha matusi kuwafurahisa Wazungu
 
Maadili ya Nchi ni muhimu sana kuliko mgombea mmoja anayeporomosha matusi kuwafurahisa Wazungu

Kujipa mamlaka ya kuona kipi ni muhimu zaidi kwa watu, ni ushahidi tosha kuonyesha kuwa mengine haya ya matusi na hata hao unaoita wazungu, ni visingizio tu baada ya kuzidiwa kwenye ulingo wa kampeni.

Kwani wananchi ni wajinga kutokuona nani ni wa matusi ili wamchague tu asiyekuwa wa matusi?
 
Ingawa hiyo ccm inabebwa kwa kila kitu! katika hali isiyo ya kawaida na ya kushangaza, mgombea wao pumzi imekata mapema kabisa!!

Yupo kwenye mapumziko ya lazima ili kupanga mikakati na mbinu za namna ya kumkabili yule jamaa machachari wa Chadema.
 
Zitto , Kinana ,Nape.nk

Wamesema "tumewakabidhi nchi washamba na malimbukeni" ndio tunaona faida zake.

Dikteta uchwara

Tanzania mpya inahitaji kuzaliwa sasa. Tanzania ambayo itaweka haki na uhuru wa watu kama mambo ya msingi mno. Tanzania itakayotambua kuwa kila mtu atakuwa huru na mwenye haki sawa siku zote.

Tanzania hiyo itaweka mamlaka zote yaani polisi, tume, mahakama, vyombo vya habari nk kujikita katika kuhakikisha kuwa haki na uhuru wa watu vinatamalaki.

Katika Tanzania hiyo wagombea wote watakuwa na haki, fursa na uhuru sawa mbele za wapiga kura.

Kwa hakika maisha yatakuwa murua.
 
Zitto , Kinana ,Nape.nk

Wamesema "tumewakabidhi nchi washamba na malimbukeni" ndio tunaona faida zake.

Dikteta uchwara

Huyu bwana angepumzika mwenyewe badala ya kusubiria aibu ya sanduku la kura.

Bahati mbaya waliomzunguka hawamwambii kuwa katika timu ya wanaochukiwa mno hapa nchini hawezi kukosa namba.

Heko makondakta na masupika wetu maana humo nanyi ni wacheza wa kulipwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…