Kampeni chafu zaanza UVCCM

Kampeni chafu zaanza UVCCM

Some of us will soon be proved right. unahitaji moyo wa paka kutetea mambo mengine. Hata hivyo kinachogomba hapa nafikiri ni nani anapokea zaidi kuliko anayetoa huo msaada. Angekuwa anapokea dagaa tu duh JF hapangetosha lakini anayepokea, loh.... funika kombe. JF inapoteza hadhi, koleo haliitwi tena koleo, na nyani anaangaliwa kwanza sura lakini thubutu utamke hivyo. Hivi akina Lowassa, Mkono na hata Mkapa wameshitakiwa ? ..ama kweli, wanavyovaliwa njuga humu JF !!! Kichwa kimenasa, juhudi za kuokoa zapamba moto.... kulikoni ? Sasa ni wakati mwafaka wa kutamka wazi kuwa CCM imeoza, full stop.
 
Mkuu Mtanzania,

Tuache ubaguzi jamani, tuache kuhukumu bila ukweli tusichukie wanaanchi wenzetu kwa sababu ni matajiri tu kutoa kwake sio dhambi, kama ana dhambi isemwe hapa lakini tuache hisia kwa sababu ni Mhindi.

Haiwezekani rais akaamuru wahalifu wa EPA, wafikishwe kwenye sheria halafu akarudi kuchukua hela za wahalifu wengine, tusilazimishe tu kwa nguvu uhalifu kwa wananchi kwa sababu hatufanani nao, sio vizuri kwa mshikamano na amani ya taifa letu jamani!

Hili siyo swala la ubaguzi kwamba tunamjadili huyu kwa kuwa ni mhindi, bali tunamjadili huyo kwa kuwa ana tuhuma nzito dhidhi yake katika ufisadi wa ununuzi wa Rada. Huku ni kukumbatia mafisadi na ndiyo maana ufisadi utaendelea kushamiri Tanzania. Usilifananishe hili na ubaguzi hata kidogo. Utajiri wanaoupata kwa kupitia njia za haramu si utajiri unaostahili kupigiwa makofi hata siku moja.
 
Ndugu yangu FMES,

Naamini tunakubaliana kwenye mambo mengi tu ila moja tu kubwa nalo ni namna ya kupambana na maadui wa taifa letu. Wewe ni mwana CCM na bado una imani kuwa yote yawezekana ndani ya CCM. Mimi kwa upande wangu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na ni mhitimu tu wa elimu ya sekondari ambacho kwa kiwango cha shule ni kama sijasoma. Nimebahatika tu kwa kujiendeleza na kwa utundu wangu nimeweza kujua kuitumia tovuti na sina utaalamu zaidi ya hapo. Kutofautiana na siasa za kwetu toka umri mdogo kulinifanya niache shule mapema na sasa baada ya miaka hamsini na ushenzi bado msimamo wangu ni ule ule. Sina nia nyingine zaidi ya kuungana na yeyote yule kutetea maslahi ya nchi yangu ninayoipenda Tanzania. Lakini amini usiamini mimi siye unayemfikiria - sina ubia na mtu yeyote humu ndani kwa sababu mbili. Kwanza simfahamu member yeyote wa JF na pili nina hakika hakuna member anayenifahamu hata tukikutana uso kwa uso. Naheshimu sana msimamo wako kwa issues mbali mbali ila hofu yangu ni unavyoonyesha kukerwa na misimamo tofauti na yako. Sisi sote ni binadamu na hakuna aliye perfect - at the end of the day tunajikuta wote ni Watanzania wanaopigania the very best for our country. Asante Mkuu, mag3.
 
Habari ulioyileta mwenyewe hapa JF inasema hivi huyu Somaiya sio mshitakiwa ila rafiki yake ndiye, sasa ninauliza swali kosa la huyu Mhindi tajiri ni lipi hasa mpaka kuzua maneno yote haya yenye hasira na chuki za nguvu?

Ni lini Tanzania tumeanza kukataa misaada kutoka kwa wananchi? Mboan siku zote sisi ni watu wa misaada tu, sasa hapa kuna hasira sana kwani huyu mhindi kosa lake ni nini hasa?

Wakuu naomba niwaachie huu mjadala naona unaanza kwenda kusikofaa, nilitaka kujua tu kosa la huyu mtoa msaada na kosa la kupokea kwa CCM, ahsante kwa darasa zito sana.
 
Ndugu yangu FMES,

Naamini tunakubaliana kwenye mambo mengi tu ila moja tu kubwa nalo ni namna ya kupambana na maadui wa taifa letu. Wewe ni mwana CCM na bado una imani kuwa yote yawezekana ndani ya CCM. Mimi kwa upande wangu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na ni mhitimu tu wa elimu ya sekondari ambacho kwa kiwango cha shule ni kama sijasoma. Nimebahatika tu kwa kujiendeleza na kwa utundu wangu nimeweza kujua kuitumia tovuti na sina utaalamu zaidi ya hapo. Kutofautiana na siasa za kwetu toka umri mdogo kulinifanya niache shule mapema na sasa baada ya miaka hamsini na ushenzi bado msimamo wangu ni ule ule. Sina nia nyingine zaidi ya kuungana na yeyote yule kutetea maslahi ya nchi yangu ninayoipenda Tanzania. Lakini amini usiamini mimi siye unayemfikiria - sina ubia na mtu yeyote humu ndani kwa sababu mbili. Kwanza simfahamu member yeyote wa JF na pili nina hakika hakuna member anayenifahamu hata tukikutana uso kwa uso. Naheshimu sana msimamo wako kwa issues mbali mbali ila hofu yangu ni unavyoonyesha kukerwa na misimamo tofauti na yako. Sisi sote ni binadamu na hakuna aliye perfect - at the end of the day tunajikuta wote ni Watanzania wanaopigania the very best for our country. Asante Mkuu, mag3.

Hapa unajiandikia na kujijibu mwenyewe au umechanganya data za User name katika ku log in?
 
Hapa unajiandikia na kujijibu mwenyewe au umechanganya data za User name katika ku log in?

Haya yalikuwa ni mawasiliano yangu na FMES kwenye PM. Naona ameamua kuyaweka hadharani - sababu anazijua mwenyewe. Hata hivyo namshukuru kwa kuyaweka hadharani.🙄😱😉🙂
 
Some of us will soon be proved right. Inahitaki moyo wa paka kutetea mambo mengine. Hata hivyo kinachogomba hapa nafikiri ni nani anapokea zaidi kuliko anayetoa huo msaada. Angekuwa anapokea dagaa tu duh JF hapangetosha lakini anayepokea, loh.... funika kombe. JF inapoteza hadhi, koleo haliitwi tena koleo, na nyani anaangaliwa kwanza sura lakini thubutu utamke hivyo. Hivi akina Lowassa, Mkono na hata Mkapa wameshitakiwa ? ..ama kweli, wanavyovaliwa njuga humu JF !!! Kichwa kimenasa, juhudi za kuokoa zapamba moto.... kulikoni ? Sasa ni wakati mwafaka wa kutamka wazi kuwa CCM imeoza, full stop.

Ndugu yangu FMES,

Naamini tunakubaliana kwenye mambo mengi tu ila moja tu kubwa nalo ni namna ya kupambana na maadui wa taifa letu. Wewe ni mwana CCM na bado una imani kuwa yote yawezekana ndani ya CCM. Mimi kwa upande wangu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na ni mhitimu tu wa elimu ya sekondari ambacho kwa kiwango cha shule ni kama sijasoma. Nimebahatika tu kwa kujiendeleza na kwa utundu wangu nimeweza kujua kuitumia tovuti na sina utaalamu zaidi ya hapo. Kutofautiana na siasa za kwetu toka umri mdogo kulinifanya niache shule mapema na sasa baada ya miaka hamsini na ushenzi bado msimamo wangu ni ule ule. Sina nia nyingine zaidi ya kuungana na yeyote yule kutetea maslahi ya nchi yangu ninayoipenda Tanzania. Lakini amini usiamini mimi siye unayemfikiria - sina ubia na mtu yeyote humu ndani kwa sababu mbili. Kwanza simfahamu member yeyote wa JF na pili nina hakika hakuna member anayenifahamu hata tukikutana uso kwa uso. Naheshimu sana msimamo wako kwa issues mbali mbali ila hofu yangu ni unavyoonyesha kukerwa na misimamo tofauti na yako. Sisi sote ni binadamu na hakuna aliye perfect - at the end of the day tunajikuta wote ni Watanzania wanaopigania the very best for our country. Asante Mkuu, mag3.
 
Mkuu Mtanzania,

Tuache ubaguzi jamani, tuache kuhukumu bila ukweli tusichukie wanaanchi wenzetu kwa sababu ni matajiri tu kutoa kwake sio dhambi, kama ana dhambi isemwe hapa lakini tuache hisia kwa sababu ni Mhindi.

Haiwezekani rais akaamuru wahalifu wa EPA, wafikishwe kwenye sheria halafu akarudi kuchukua hela za wahalifu wengine, tusilazimishe tu kwa nguvu uhalifu kwa wananchi kwa sababu hatufanani nao, sio vizuri kwa mshikamano na amani ya taifa letu jamani!

Mkuu FMES,

Kwa mazingira ya TZ hata wengine tuna visenti vyetu hata kama sio vingi kwi kwi kwi!!. Suala hapa ni kuchukia maovu na wala sio kuchukia utajiri.

Mtu anayepata utajiri wa kihalali unafikiri ataenda kutoa CCM milioni 400?

Kama anazo na anataka kusaidia kuna miradi chungu nzima ya maendeleo ya nchi.

Unaongelea ubaguzi wakati hapa hatujadili rangi waka kabila lake. Tunajadili jinsi mafisadi wanavyojipenyeza kupitia mlango wa vyama vya siasa.

Hao jamaa hawana lolote la maana zaidi ya kununua wanasiasa wetu. Ukiwa mwanasiasa makini, kaa mbali na tamaa za matajiri.

Leo mwambie Mbowe akaombe mcahngo kwao, hatapata kitu lakini kesho akishinda urais hao hao ndio wa kwanza kwenda kujigonga gonga na kuahidi michango kibao.

Aibu kweli kweli hata kwa huyo JK mwenyewe kuchekelea hao majambazi ambao kila siku wanakwepa kulipa kodi.

CCM ina wanachama wa kutosha kuiendesha, hivi kweli wanahitaji hizo pesa za hao mafisadi? Kweli wanahitaji mkutano mkubwa kiasi hicho? Jamaa wanaiba kwenye radar, huku wanajifanya wanatoa kwa mkono mwingine. Hao ni conmen tu ambao wanajipitisha pitisha kwa wanasiasa ili kupata favours.
 
Huyu naye ni rafiki wa Somaiya or what?

Maana yangu ilikuwa kuonyesha gharama ambazo nchi inakuja kubeba baadaye kwa sababu ya kuendekeza huu ubia wa CCM na wafanyabiashara ambao hautawaliwi/kuendeshwa na miiko au sheria yeyote.
 
Hebu tujikumbushe kidogo ya nyuma ......................

Tanzanian tycoons divulge getting $12m secret payout
2007-01-16 10:15:02
By London

TwoTanzanian business moguls have admitted they were secretly paid $12m/- by UK`s biggest arms supplier in a controversial deal in, which Tanzania bought an obsolete military radar system.

The tycoons, Sailesh Vithlani and business partner, Tanil Somaiya made the admission to British detectives who recently flew into the country to investigate graft allegations in the controversial sale of the radar by BAE.

Vithlani, who acted as a middleman in the deal and has a long-standing relationship with military and government figures, has admitted that the sum was covertly moved to a Swiss account by BAE Systems, which is under investigation by the Serious Fraud Office.

The SFO, which was recently forced to abandon its investigation into commissions paid on a massive arms contract with Saudi Arabia, is now focusing its attention on Tanzania.

The back-door payment represented 30 per cent of the contract value. Tanzania had to borrow to finance the deal, which critics said was unnecessary and overpriced.

The duo is expected to act as prosecution witness in the BAE`s corruption case.

In Dar es Salaam, Vithlani`s business partner, Tanil Somaiya, told the London Guardian that British police had already flown out to trace and interview both men as potential witnesses.

The admissions by Vithlani, has led to calls in London for BAE's prosecution if the allegations were proved.

Vithlani was the majority shareholder in Merlin International Limited, Somaiya said, while he had a small token interest himself. BAE paid $400,000 down this route in stage payments, Somaiya said, as the radar equipment was delivered.

Vithlani acted as agent not only on the radar deal but also in the 2002 purchase from the US of a top-of-the-range Gulfstream official jet for the then Tanzanian president, Benjamin Mkapa, at a cost of more than $40m.

Police sources in Dar es Salaam said the agreement to use Vithlani as an agent had been signed off by the then chairman of BAE, Sir Dick Evans.

Sir Dick, who has been at the centre of many of the arms deals under investigation, has already been interviewed by the Serious Fraud Office during their two-year inquiry.

When asked about the BAE money, Vithlani told the Guardian he had made no disbursements from the Swiss cash to public officials in Tanzania. Asked if he had disbursed any of the $12m to third parties outside of Tanzania, he declined to comment.

"When the UK police travelled to Tanzania, we met them at their request and answered all their questions," he said.

At the same time, it has emerged that British Premier, Tony Blair supported the 2002 sale, a move that was fiercely opposed by former cabinet minister Clare Short and the chancellor, Gordon Brown.

Clare Short said the prime minister had been personally responsible for forcing the licence for the Tanzania deal through the cabinet. "It was always obvious that this useless project was corrupt," she said.

He said BAE had made two parallel arrangements with the middlemen. In the first, a conventional agency agreement was signed.

Under this, 1% commission was to be paid if the $40m radar deal went through, to a Tanzania-registered firm, Merlin International Ltd.

But under a second, more unusual agreement, BAE`s secretly owned offshore company Red Diamond deposited another $12m, representing 30% of the contract price, in Switzerland.

That money was under the personal control of Vithlani, Somaiya said, and this had been admitted to UK police.

When asked if he would allow British police to inspect all the transactions on his Swiss account, he declined to comment.

In the secretive world of international arms deals, a commission of 1% to local agents would generally be regarded as legitimate.

The government's export credit agency, the Export Credits Guarantee Department, has guidelines under which a ``commission`` of more than 5-10% is automatically regarded as questionable.

BAE System's payment of as much as 30%, coupled with the use of a Swiss bank account and apparent double sets of agency agreements, would normally arouse suspicions of possible bribery, investigators say.

BAE Systems were yesterday asked why they had made a 30% payment to Vithlani`s Swiss account.

The company refused to answer, saying: "We will not be commenting on any point of substance. This cannot of course be taken as any kind of admission."

The SFO also refused to discuss their investigation. President Jakaya Kikwete, is due in London today to speak at a meeting with Hilary Benn, the international development secretary, on efforts to overcome corruption in Tanzania.

Later this week, the UK is expected to have to defend its actions over BAE at a meeting of the anti-bribery group of the OECD in Paris.

Leo T. Somaiya anaichangia CCM. Ingekuaje mchangiaji angekuwa Chenge. Wote bado ni watuhumiwa tu na wote wana mamilioni nje.
 
Source: This Day.

Vithlani has since been charged at the Kisutu court with committing perjury and making false statements to an investigating officer, with prosecutors alleging that he lied about not being the owner of Envers Trading and about receiving a $390,000 commission for the radar deal while he was actually paid $12m. The fugitive businessman was charged in absentia and remains at large, despite an international arrest warrant issued for him.

However, despite reportedly severing all his business ties with Vithlani, Somaiya was business a partner with the wanted fugitive at the time the radar deal was concluded. It remains uncertain whether or not authorities consider him a formal suspect in the ongoing radar investigation.
 
hii kali!! Na huyu somaiya akiwa kwenye issue ya epa watamkamata kweli?

mara mbili?..huyu yupo share na yule aliyeliuzia jeshi letu helixopter feki za augusta bell..zinazoangoka na kuuwa askari wetu kila siku..alipewa oda ya helicopter 6....kaleta 4 tu...na kati ya hizo 2 zimeanguka ndani ya miezi 6..ikiwemo iliyoanguka baada ya kumaliza doria ya sulivan...zimebaki 2..zipo grounded ..ma pilot wanaziogopa...mbili zingine hadi leo hajaleta ili kutimiza idadi ya sita...nadhani hizo ndio imetoka!!!!!

Sasa milioni 400 na bilioni zaidi ya 60 alizotengeneza kwa kuuza helicopter feki wapi na wapi!!??...alafu ndio "
kujitangaza kibiashara huko?"
 
Mkuu ni kweli kabisa kua enzi za mwalimu huyu asingesogea kabisa kwa sababu ya kuhisiwa tu, maana kulikuwa hakuna sheria enzi hizo, sheria ilikuwa ni yeye Mwalimu,

lakini je unajua enzi za mwalimu CCM walikuwa wanatoa wapi hela za kuendesha chama? angalau siku hizi tunajua kuwa wana ruzuku!

Mtamsingizia vingi Mwalimu (Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) Ha ha ha ha eti wakati wa Mwalimu kulikuwa hakuna sheria ndiyo maana hawa mafisadi na mabulungutu yao waliogopa kuisogelea CCM ili kutoa misaada ya mabulungutu yao!!! Kama sheria ilikuwa ni yeye Mwalimu tu basi majaji, Mahakimu na wanasheria wangeshalalamika kwamba Mwalimu anawaingilia kwenye kazi zao!!! Na kuwataka kila kesi waamue alivyotaka yeye Mwalimu!!!! lakini hatukusika hata mara moja malalamiko yao!!! Mwalimu hakuwa perfect lakini msimsingimzie vya kumsingizia!!!!

Na siku hizi kwa kuwa tuna sheria nzuri sana Tanzania mafisadi hawaogopi tena kuisogelea CCM na kutoa mabulungutu yao!!! 😕

Hivi umesahau kama TANU na CCM ya Mwalimu ilikuwa inaendeshwa kwa ada toka kwa wanachama!? Wakati ule Watanzania wengi tuliona fahari kutoa ada zetu za kila mwezi maana tuliona chama kimeweka mbele maslahi ya Watanzania na siyo wageni ama mafisadi kama ilivyo hivi sasa na matokeo yake Wanachama wengi siyo hai tena maana hawatoi ada zao. Au huna 'data' za kukumbuka hayo!?
 
Mtamsingizia vingi Mwalimu (Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) Ha ha ha ha eti wakati wa Mwalimu kulikuwa hakuna sheria ndiyo maana hawa mafisadi na mabulungutu yao waliogopa kuisogelea CCM ili kutoa misaada ya mabulungutu yao!!! Kama sheria ilikuwa ni yeye Mwalimu tu basi majaji, Mahakimu na wanasheria wangeshalalamika kwamba Mwalimu anawaingilia kwenye kazi zao!!! Na kuwataka kila kesi waamue alivyotaka yeye Mwalimu!!!! lakini hatukusika hata mara moja malalamiko yao!!! Mwalimu hakuwa perfect lakini msimsingimzie vya kumsingizia!!!!

Na siku hizi kwa kuwa tuna sheria nzuri sana Tanzania mafisadi hawaogopi tena kuisogelea CCM na kutoa mabulungutu yao!!!

Hivi umesahau kama TANU na CCM ya Mwalimu ilikuwa inaendeshwa kwa ada toka kwa wanachama!? Wakati ule Watanzania wengi tuliona fahari kutoa ada zetu za kila mwezi maana tuliona chama kimeweka mbele maslahi ya Watanzania na siyo wageni ama mafisadi kama ilivyo hii leo. Au huna 'data' za kukumbuka hayo!?

Maneno umesema mengi sana lakini hayana uhusiano wowote na CCM kupokea msaada wa mwananchi, semeni labda tatizo ni kwa sababu ni Mhindi, dataz nilizonazo ni kwamba CCM enzi hizo ilikuwa haina bajeti wala responsibility, ilikuwa inachota tu serikalini bila idhini yetu wananchi, Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu pia, lakini no way ninataka kurudi kwenye maisha yake tena yale ya foleni za unga wa njano no thank you!

Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!

Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.
 
Ha ha ha ukiwauliza Watanzania walio wengi watakwambia tulikuwa na utawala bora wakati wa Mwalimu kuliko sasa. Mwalimu asingekubali mafisadi wa EPA waendelee kupeta bali angewasweka rumande wakati uchunguzi mkali unaendelea. Mwalimu asingekubali kusaini mikataba ya uchimbaji wa madini ambayo Watanzania tunaambulia asilimia tatu tu kama alivyofanya fisadi Mkapa na Kikwete pamoja na kuahidi kuipitia tena mikataba hiyo hadi hii leo miaka mitatu madarakani hajafanya lolote kutimiza ahadi yake. Kwa hiyo uliyoyaona wewe wakati wa Mwalimu ni foleni za unga wa njano tu!!!! Hukumbuki kwamba wakati Mwalimu anaingia madarakani tulikuwa hatuna chuo kikuu na vyuo vya kati. Akajenga UDSM, IFM, Nyegezi, IDM. Hukumbuki tulikuwa hatuna viwanda akajenga viwanda mbali mbali ambavyo viliajiri Watanzania katika nafasi mbali mbali hata zile za juu. Hukumbiki kwamba tulikuwa hatuna lugha ya Taifa na kwa msisitizo wake akaona kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na lugha yetu ya Taifa ili kuwaunganisha Watanzania wote na ndiyo maana Watanzania wengi pamoja na kuwa Mwalimu hakuwa perfect lakini tunajua siku zote aliweka maslahi ya Watanzania mbele na hakuwa na tamaa ya utajiri wa haraka haraka wala hakuwa fisadi na ndiyo maana wengi tunamuenzi hadi hii leo lakini unachokumbuka wewe ni foleni za unga wa njano tu!!!!!.

Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!!

Huo uwananchi wa wahindi akina Manji, Rostam, Somaiya umekuwa na umuhimu mkubwa miaka hii!!! Wakati wa Mwalimu hawakuona umuhimu wa wao kuwa Watanzania!!! Hadi hivi sasa!!! Kwa sababu zipi!? 😕

Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.

Hivi unaamini kweli msaada wa Somaiya unasaidia Taifa!!!? Kivipi!? 😕 Kama alikuwa anataka kusaidia Taifa kwa nini asitumie mapesa yake hayo kununua vitanda vya wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, Temeke, Amana, Mwananyamala na mahospitali mengine ambako wagonjwa chungu nzima wakiwemo akina mama wajawazito au waliotoka kujifungua wanalala chini? Kwa nini asinunue madawati katika shule ambazo wanafunzi wanakaa chini au kwa kwenye matofali!? Kwa nini asinunue vifaa muhimu vya mashuleni kama vile vitabu, chaki ili kupunguza upungufu mkubwa wa vifaa hivyo muhimu? Fungua macho kaka hawa ni mafisadi tu wanaotumia mapesa yako ili siku ya siku waje kukingiwa kifua na wanene kama wangekuwa wanataka kuwasaidia Watanzania wanajua ni wapi pa kuelekeza misaada yao.
 
This is completely Madness,

Yaani ukiangalia sura zao wote kuanzia Raisi, Msekwa, Nchimbi n.k unaweza kutabiri wanawaza nini moyoni '''lete hiyo pesa wee ....""

Ukimwamgalia Rostam Aziza utagundua anawaza .... Duuu ningekuwa mimi ndio natoa hiyo zawadi... duu...jamaa amenizidi hesabu.

Huuu ni upu.mbavu wa hali ya juu wa viongozi wetu.

sasa kuna kosa gani kusema CCM ni chama cha majambazi.???
 
Lakini Tajiri Soros mbona amewahi kutumia dola millioni 20 kusaidia Democrats huko USA, hasa kwenye uchaguzi dhidi ya Bush kwenye term ya pili?

Hapa sidhani kama tatizo ni kutolewa kwa hela, au kwa CCM kupokea hizo hela, labda tatizo ni mtoaji anataka nini au amewahi kutaka nini au amewahi kupewa nini na watawala wetu, kama yanafahamika yawekwe wazi hapa otherwise tusiwakatishe tamaa wananchi wenye nia ya kutoa misaada kusaidia vyama vyetu vya siasa.

Kutoa misaada kwa vyama vyetu vya siasa sio kuvunja sheria ya jamhuri yetu, au?

Hauwezi ukalinganisha moja kwa moja mazingira ya misaada ya uchaguzi kati ya Tanzania na Marekani, Marekani kuna level ya hali ya juu sana ya 'Transparency', Hapa Tanzania bado tuko kwenye giza nene hasa hasa kwa upande wa kuwafaham hao watu wanapata wapi hizo pesa na nia yao ya kuchangia,
 
Date::11/10/2008
Mfanyabiashara atoa Sh400milioni kugharimia mkutano UVCCM

Na Daniel Mjema, Dodoma

MFANYABIASHARA mashuhuri nchini, Tanil Somaiya anayemiliki Kampuni ya Shivacom ametoa Sh400 milioni kugharamia Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Mfanyabiashara huyo alikabidhi msaada huo unaohusisha vifaa vyenye thamani ya Sh250 milioni na fedha taslimu Sh150 milioni za posho za wajumbe wanaokadiriwa kuwa 1,000, kwa Mwanyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete katika tafrija fupi iliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma.

Kabla ya kukabidhiwa kwa msaada huo, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Issack alisema katika kufanikisha mkutano huo wa uchaguzi, Baraza Kuu la UVCCM liliamua kuteua kamati maalumu ya watu wanne ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma William Lukuvi, kutafuta fedha.

Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Lawrence Masha, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Somaiya.

Issack alisema Baraza Kuu la UVCCM liliwaagiza kutafuta vifaa 1,000 kila kimoja ambavyo ni pamoja na fulana, kofia, mabegi, kalamu na madaftari ambavyo vilitengenezwa kwa gharama ya Sh250,000 katika kiwanda kinachomilikiwa na Somaiya mwenyewe.

Kwa mujibu wa kaimu katibu huyo, ingawa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa ni 750 lakini wapo waalikwa ambao ni pamoja na Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambao pamoja na wajumbe wengine watalipwa posho ya Sh50,000 kwa siku.

Akikabidhi msaada huo, Somaiya alisema ameamua kukisaidia chama hicho kwa kuwa yeye ni mkereketwa na mpenzi wa CCM, kauli ambayo ilipongezwa na Rais Kikwete ambaye alisema kwa kutoa msaada huo, mfanyabiashara huyo atakuwa amejitangaza kibiashara.

Tafrija hiyo fupi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa NEC waliomaliza kikao chao jana mchana na kupitisha majina ya wanachama wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi UVCCM, Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi.

Katika hatua nyingine, wazee wa CCM wa wilaya ya Dodoma mjini wamemuomba Rais Kikwete kuharakisha mpango wake wa kupitisha utaratibu unaotenganisha suala la uongozi na biashara ndani ya Serikali na ndani ya chama cha Mapinduzi.

Akisoma risala kwa niaba ya wazee hao Ikulu ndogo mjini Dodoma jana, Mohamed Makbel alisema bila maadili hakuna nidhamu na kutaka linalowezekana leo lisingoje kesho.

“Pamoja na hayo ili kulinda umoja wetu tunaomba viongozi wetu wa chama na serikali wanapotofautiana watumie vikao husika vya chama,” ilisema sehemu ya risala hiyo.

Pia waliomba kupitiwa kwa sheria ya mwaka 1979 iliyoagiza Dodoma kuwa eneo maalumu la uwekezaji ili sheria hiyo ihuishwe kuwawezesha wawekezaji wengi kuwekeza Dodoma na kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha usambazaji wa bidhaa mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Walimpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa ujasiri wa kuamua kujenga chuo kikuu cha Dodoma na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa ndege wakisema uamuzi huo umeongeza shauku kubwa ya maendeleo ya kiuchumi ya mkoa huo wa Dodoma.

Akiwahutubia wazee hao, Rais Kikwete alisema azima ya serikali ya makao makuu kuhamia Dodoma iko palepale na kwamba amefarijika na hotuba ya wazee hao kwani imeonyesha namna ambavyo bado wako pamoja na serikali yao katika kupigania maendeleo ya wananchi.

Kuhusu suala la kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa eneo huru la kibiashara, Rais alisema utekelezaji wa suala hilo ulikwishaanza japo kasi yake haiendi kama ilivyotarajiwa lakini aliahidi kuwa serikali italitazama suala hilo ili shabaha iliyokusudiwa na Serikali iweze kufanikishwa.

Baada ya kuwakana wafadhili wa EPA SSM imeshajua fika kuwa 2010 hawatakubali kuchangia hivyo inaanza kuwatafuta wapya wakiwemo wahindi maana ndo wanataka kujipendekeza maana ssm imewalea na kuwaimarisha kifedha. Kwa mantiki hiyo wahindi wanahakikisha at any cost ni lazima ssm iwe madarakani ili ilinde maslahi yao.

Hapo hapo wale wahindi wengine ambao walikuwa havumi wanatumia hili la EPA ili waweze kujipenyeza kwa ssm nao wafaidi nchi kwa vifua. vya ssm

Kwa namna hii wakuu wazalendo au wenye nchi hatutakaa tunyanyuke. Kwa mawazo yangu naona kuwa serikali imeweka wageni mbele na kusahau wenye nchi. Kweli waswahili husema"Mkono mtupu haulambwi".

Subash Patel naye sijua atachangia kiasi gani?????!!!!! Ila huyu ni mjanza sana na subirini hapo UVCCM watakaposhindwa masharti ya mkataba wa kitapeli uone jinsi atakavyowahi mahakamani kufungu kesi ya madai na achukuwe jengo na kila kitu. Yangu macho!!!

Ati kumpa Somaiya nafasi ya kujitangaza kibiashara!!!!! Kwani nini asitangaze biashara za wafanyabiashara wazalendo na si za hao wenye uraia nne?? Ati tunazungumzia masuala ya uwezeshaji wananchi kwa kuwadanganya kuwapa vimkopo vya sh. laki moja eti aendelee???????? Ningefurahi kama angekuwa anatangaza biashara ya mzalendo ambao wengi hata fedha yao iko hapa nchini na pengine wewe na mimi tumeshaenda benki kukopa ikiwa ni depostis zao kuliko hizo za wahindi zinazohifadhiwa mabenki ya kwao au nchi nyinginezo na maltiplier effect yao ni zero kwa uchumi wetu!!!!!
 
Maneno umesema mengi sana lakini hayana uhusiano wowote na CCM kupokea msaada wa mwananchi, semeni labda tatizo ni kwa sababu ni Mhindi, dataz nilizonazo ni kwamba CCM enzi hizo ilikuwa haina bajeti wala responsibility, ilikuwa inachota tu serikalini bila idhini yetu wananchi, Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu pia, lakini no way ninataka kurudi kwenye maisha yake tena yale ya foleni za unga wa njano no thank you!

Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!

Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.

FMES,
Siamini kama unaamini kuwa kula unga wa njano ulitokana na Mwalimu kuwa RAIS wetu wakati ule! Haujawahi kuliweka wazi tatizo lako na Mwalimu.
 
Back
Top Bottom