hapa Arusha Chadema na CCM hawa wengine wana sindikiza tu
Heshima kwako Crashwise,
Mkuu hii ni habari nimeinyofoa Tanzania Daima gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa hebu soma bila ushabiki maandazi unaotaka kuuleta jamvini.Mkuu najua unapenda Godbless lakini anaendekeza upuuzi kwa namna ya ajabu kiasi kwamba baadhi ya wapenzi wake wameanza kumkimbia.Mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Themi Bwana Ngowi juzi alipata wakati mgumu kumtetea Godbless ofisi za TANESCO mkoa baada ya baadhi ya watu kumuuliza imekuwaje mtu kama yeye mwenye elimu nzuri kama yeye asigombee ubunge na kumwacha Lema mwenye elimu ya ndogo na uelewa mdogo akikidhalilisha chama.Kwa taarifa yako mpaka sasa Lema ana kesi kumi na moja nyingi ni za utapeli na kutishia watu maisha.
Kampeni Arusha Mjini zapata moto
na David Frank, Arusha
KAMPENI za kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini zimezidi kuchukua sura mpya kwa wagombea kujinadi kwa staili tofauti ikiwa ni pamoja na kupigana vikumbo misibani, huku wengine wakijinadi katika vijiwe vya kahawa na vibanda vya kung'arishia viatu. Hali hiyo inadhihirisha kuwa kampeni za majukwaani na zile za nyumba kwa nyumba bado hazitoshi kufuatia kuwepo na msuguano mkali baina ya wagombea kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Labour (TLP) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Tukio la aina yake lilitokea juzi katika msiba wa mfanyabiashara maarufu Naftal Mollel eneo la Kaloleni jijini hapa na baadaye mazishi kufanyika Kijenge ambapo mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Godbless Lema, alishiriki katika mazishi hayo huku akionekana kutumia muda wake vizuri kwa kunadi sera zake.
Wakati mgombea huyo akiendelea kumwaga sera zake, ghafla mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, aliingia katika mazishi hayo akiongozana na wapambe wake na mara msiba huo ukageuka kuwa furaha baada ya waombolezaji kufurahia ujio wake na kusahau majonzi ya ndugu yao.
Mgombea huyo alianza kuwapa mkono wa pole ambapo waombolezaji hao kwa upande wao walijikuta wakiimba ‘daada…daada….daada' na kufanya umma uliokuwa umefurika katika mazishi hayo kutaharuki.
Lakini wakati hayo yakitokea, mgombea kiti hicho kupitia TLP, Macmillan Lyimo, ambaye amepanda chati siku za hivi karibuni na kutishia nafasi za wagombea wengine, amekuwa akimwaga sera zake katika vijiwe mbalimbali jijini hapa vikiwemo vibanda vya kung'arishia viatu na vya kahawa.
Tanzania Daima ilishuhudia mgombea huyo akimwaga sera zake katika vibanda vya kung'arisha viatu karibu na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Mji Kati akiwaomba wang'arisha viatu kumpa kura ili alete mabadiliko na kulipatia jimbo la Arusha maendeleo ya kweli.