Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Nimejawa na furaha ya ajabu mchanawa leo kwa mara ya kwanza nimepokea barua pepe kutoka international criminal court(ICC).
Mnamo tarehe 27/08/2013 nilituma barua pepe kwenda ICC nikiomba ufanyike uchunguzi juu ya mauaji yanayoendelea Tanzania ikihusisha jeshi letu la polisi.
Ktk kutia uzito nilituma maelezo marefu nikiambatanisha video na picha katika matukio mbalimbali kuanzia:
-Tukio la kuuawa Daudi Mwangosi, Nyororo-Iringa,jioni ya tarehe 02, septemba 2012 (niliambatanisha na picha),
-Tukio la mauaji ya Songea, polisi walipopiga risasi raia kama wanaua digidigi, tarehe 22,februari 2012 (niliambatanisha na picha),
-Mauaji ya Arusha, wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Januari 05, 2011 (niliambatanisha video),
kwa ufupi polisi kwa mwaka 2012 pekee wameua raia 20 ktk mikoa ya Ruvuma, Mara, Dar es Salaam, Morogoro na Kagera pekee.
Niliandikia kitengo cha uchunguzi nikitarajia kuwa sitojibiwa lakini nilijibiwa nikiambiwa kuwa watafanyia kazi na watanijibu. Imenipa faraja sana kwa kweli. Tumepata mwanzo mzuri.
Lakini napenda kuomba kwa wale wanaoitakia mema nchi yetu na wenye kukerwa na namna polisi walivyogeuka miungu watu, wanavyoua raia.
Tutume ujumbe wa kutosha kwenda ICC kitengo cha uchunguzi tukiomba kufanya uchunguzi kwa tuhuma za uvunjaji wa haki za binadamu/makosa dhidi ya uhalifu wa kibinadamu(crimes against humanity).
Watuhumiwa wakubwa ni Jakaya Mrisho kikwete, IGP Saidi Mwema na Kamanda Michael Kamuhanda,
Tutume ujumbe wa kutosha ili kuwaamsha ICC, Huku tukitoa vielelezo namna walivyohusika na mauaji ya raia.
Tuma vielelezo vya picha au/na maelezo kwenda kitengo cha uchunguzi wa mashtaka ICC kwa anuani hizi hapa;
Information and evidence unit office of the prosecutor, post office box 19519, 2500CM, The Hague, Netherlands.
Email: informationdesk@icc-cpi.int,
Nukushi: +(31) 705158555.
Tafadhali jitahidi kutuma pasipo kujali itikadi ya chama chako.