Bubu,Rwabugiri,Mkandara,tz-devil,KadaMpinzani,Masatu,
katika kila awamu ya serikali za Tanzania kumetokea matatizo yaliyosababisha wananchi kupoteza maisha kutokana na msuguano na vyombo vya dola.
wakati wa Nyerere wako waliopoteza maisha kutokana na operesheni vijiji. vilevile kulitokea matatizo Shinyanga. Mwinyi alipokuwa madarakani kulitokea machafuko Kilombero. Mkapa naye ktk awamu yake tumepata matatizo Mwembechai na Pemba.
Pamoja na hayo yote Maraisi wetu hawajafikia kiwango cha kuitwa WAUAJI. Vilevile Maraisi wetu hawajafikia daraja la UDIKTETA.
Hizi hoja za Mafisadi ni kama mchuzi wa Mboga. Sasa naomba waandaaji msizidishe CHUMVI mkakosa walaji. Nadhani mmenielewa.
NB:
kuna aliyedai ati pamoja na kwamba Raisi alikuwa nje ya nchi wakati wa mauaji ya Pemba, lakini anakuwa briefed. Sasa ktk mazingira kama yale ya polisi kufyatua risasi alikuwa briefed kitu gani na wakati gani?
Kwanini Mkapa ndiyo abebe lawama zote? What is Karume's responsibility in this case? How about Dr.Omar who was the acting President at the time?
Watendaji wakuu wa Polisi Zanzibar wanateuliwa na Raisi wa Zanzibar. Hata ripoti ya Hashim Mbita ilitaja majina mengi ya Makamanda wa Polisi walioshiriki na inaelekea wanatokea ZNZ.
Jokakuu,
Tatizo la mada hii ni kuwepo tuzo ambalo lkinatakiwa kupewa rais kwa sababu ya UONGOZI BORA!..
Wakati wa Nyerere watu walikufa kutokana na majanga yaliyosababishwa na siasa yenyewe! Utekelezaji wa siasa hiyo ulikuwa mbaya na siasa yenyewe lakini yote haya hayakuwa makusudio ya Nyerere wala utawala wake kuua.
Wakati wa Mwinyi pia kulitokea uzembe wa viongozi wapinzani kuuawa kwa sababu ya kupingana na mrengo wa chama. Mwinyi also was weak, kuna watu waliuawa under his watch, lakini Mwinyi hayupo ktk list ya viongozi wanaogombea tuzo ama nafasi hiyo ya Uongozi bora. Na nakuhakikishia hata kama angekuwa Mwinyi ktk nafasi hiyo ningesema ukweli daima. Kwa hiyo nachofanya mimi hapa sichagui mtu kwa jina lake ila mabaya ya Uongozi wake. Na hoja ilyopo hapa ubaoni ni TUZO hilo kama Mkapa analistahili.. nothing else!
Wapo viongozi Africa waliokuwa wabaya na walioharibu kuliko Mkapa...
mie niko tofauti na mwafrika wa kike,there iz no person who is perfect bt mkapa has done excellent in the development of this country,rejea post ya AUGUSTINE mosha alivyodadafua kati ya JK na BEN..
AS LONG AS AM A TANZANIAN,NAMSUPPORT FISADI MKAPA ,ataieletea sifa nchi yetu..
Masatu,
Mawazo yako ni yapi?... maanake sioni kitu unachoandika zaidi ya kurudia maneno ya watu na kuyaweka wino mwekundu..kisha unauliza tena kuhusu maelezo hayo ukitaka ushahidi!.. Nothing else yaani hakuna mtu hapa anayesikia hoja toka upande wako.. mathlan kama unapinga Utawala wa Mkapa kuhusika na kifo cha Dr. Omar tuambie wewe kilitokea nini kisha watu wanaweza pima uzito wa hoja yako. Otherwise sijawahi kukuona ukiandika mawazo yako mwenyewe ila kazi yako ni kupinga tuuu..kwa kunukuu maelezo ya watu wengine..
Kwa mara nyingine mjomba unachemsha wewe, Watanzania wote tunaendelea kuwaita hawa jamaa MAFISADI kwa maana tunayoifahamu sisi kwa hiyo hulazimishwi kumkubali mtu hapa sii Butiku, Mwinyi wala Mkandara.
Tanzanians bury vice-president
Tanzanians are shocked by the news
President Benjamin Mkapa and foreign dignitaries have attended the funeral of Vice-President Dr Omar Ali Juma who died of a heart attack.
Dr Juma's body, which had been lying in state in the Tanzania capital, Dar es Salaam, was flown to his native island of Pemba, where he was buried.
Flags throughout Tanzania are flying at half mast and parliament has suspended business for two days.
Sixty-year-old Dr Juma was the chief minister of Zanzibar for the ruling CCM party before moving to Dar es Salaam, to become President Benjamin Mkapa's running mate in the 1995 elections.
Masatu,
Mawazo yako ni yapi?... maanake sioni kitu unachoandika zaidi ya kurudia maneno ya watu na kuyaweka wino mwekundu..kisha unauliza tena kuhusu maelezo hayo ukitaka ushahidi!.. Nothing else yaani hakuna mtu hapa anayesikia hoja toka upande wako.. mathlan kama unapinga Utawala wa Mkapa kuhusika na kifo cha Dr. Omar tuambie wewe kilitokea nini kisha watu wanaweza pima uzito wa hoja yako. Otherwise sijawahi kukuona ukiandika mawazo yako mwenyewe ila kazi yako ni kupinga tuuu..kwa kunukuu maelezo ya watu wengine..
Kwa mara nyingine mjomba unachemsha wewe, Watanzania wote tunaendelea kuwaita hawa jamaa MAFISADI kwa maana tunayoifahamu sisi kwa hiyo hulazimishwi kumkubali mtu hapa sii Butiku, Mwinyi wala Mkandara.
Masatu said:Haya Mkandara tuletee ya kwako ya Mkapa kumuua Dr omar.....
Jamani sisi kama Watanzania -tufike mahali- tuweke utaifa wetu mbele- mengine nyuma! Watu wa mataifa mengine hawataelewa juu ya maoni kama haya!
BWM tumwombee Mungu ili atutoe kimasomaso Watanzania this time! Ishallah atapata tuzo! Dua la Kuku Halimpati mwewe!
Signature ni juu ya uadilifu ni kweli!Mzalendohalisi naomba usome tena hiyo signature yako kisha oanisha na unachotuambia hapa tafadhali.....LOL
Signature ni juu ya uadilifu ni kweli!
The issue is- BWM (mstaafu) hafai kupewa tunzo la Wastaafu Afrika kwa kuwa alikuwa sii mwadilifu!
Wastaafu wasiokuwa waadilifu Afrika ni wengi! BWM alikuwa bora kuliko akina Muluzi, n.k.
Kwa hili Watz- utaifa mbele- Tanzania BWM tumwombee kwanza ashinde tuzo! Hii ndo point yangu!
Habari za kuaminika lakini ambazo hazijathibitishwa toka katika vyanzo vyangu vya habari aliyeshinda ni Chissano. Kama kuna ukweli na habari hii basi Watanzania wapenda viongozi waadilifu watafurahia sana, kwani hakuna hata kigezo kimoja katika kuamua mshindi wa zawadi hiyo amabcho kimetimizwa na Mkapa. Na angeshinda huyu jamaa ndio kiburi kingezidi sana.
Ebu rudia kusoma maelezo yako mwenyewe kisha nambie hapa umesema kitu gani hasa!..badala ya kujibu hoja unamshambulia mtoa hoja ooh hatoi mawazo yake kazi yake kukosoa tu, kama hutaki kukoselewa iweje unakuwa mstari wa mbele kuwakosoa hao unaowaita "Mafisadi" kila uchao?
Yaani wewe naona hujui hata unachoandika! Hivi Watanzania wana sababu gani ya kumchukia Mkapa kiasi hicho!? Mbona Mwalimua aliyeng'atuka tangu 1985 miaka 22 iliyopita mpaka leo ni kipenzi kikubwa cha Watanzania walio wengi. Watanzania sio wapumbavu, Mkapa ndio aliongeza kwa kiasi kikubwa makusanyo ya kodi lakini Watanzania hawakunufaika na lolote kutokana na makusanyo hayo.
Ni kama baba anayetamba mtaani kwamba yeye ndio mwenye mshahara mkubwa pale mtaani, lakini pesa zake zote zinaishia nyumba ndogo, nyama choma na moja moto moja baridi na watoto wake wamedhoofu kwa kukosa lishe bora. Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba hakuwa Mr Clean kama alivyotaka Watanzania waamini.
Masatu,
Ebu rudia kusoma maelezo yako mwenyewe kisha nambie hapa umesema kitu gani hasa!..
Kama sitaki kukosolewa kwa nini nawakosoa hao wanaoitwa Mafisadi?.. Ni jambo gani nimewakosoa ama huelewi maana ya Kukosoa!.. Hakuna maandishi ama usemi waliotoa wenye madai tofauti na ukweli unaosemekana...
Kisha tunaoandika hapa ni sisi yaani mimi na wewe imekuwaje niwakosoe watu wasiosema ama kuandika kitu, Mjomba vipi?
Nacho kusisitiza wewe kama kweli umeongea na huyo Daktari wa marehemu na mtu wako wa karibu andika alichokuambia!..weka maandishia hapa kama sio habari za kina Sokoine, Mwaikambo, AC ambazo mnasisitiza vifo bila uchunguzi nje ya wataalam wa serikali.
Unaponiuliza mimi sababu ya serikali ya Mkapa kufanya hivyo nashindwa kabisa kukuelewa kwani hata alipofungua ofisi ya biashara Ikulu ama alipoiba fedha za Umma siwezi kujua sababu yake hasa maanake kama ni Utajiri basi fedha alokuwa akilipwa kama rais ilitosha kabisa kumtajirisha.
Kitu kimoja tu ikiwa kweli Mkapa ni mkweli na mwenye sifa usozisema mbona anashindwa kujibu tuhuma za Ufisadi akisema ni siasa!... Lini umesikia wizi wa mali ya Umma iwe siasa! na imekuwaje wanaomfuata sasa hivi ni wana CCM wenzake hizo siasa zimetoka wapi?
Bro, jaribu kuwa mkweli pale panapostahili na hata kama unapinga usiwe na lugha ya ki CCM ambayo leo hii haieweki kwa Watanzania walio wengi. Unapokana tuhuma ama mashtaka at least unakuwa na ALIBI ya wapi ulikuwa wakati tuhuma hizo zilitokea sio kukataa tu ukisema ni uongo hali ukweli pia huna.