Uchaguzi 2020 Kampeni inayosambaa Iramba ni "Kumi ya Dkt. Mwigulu Yatosha"

Uchaguzi 2020 Kampeni inayosambaa Iramba ni "Kumi ya Dkt. Mwigulu Yatosha"

Jimbo la iramba nadhani ndilo lenye mvuto wa uchaguzi wa mbuge Tanzania
 
Sijazungumzia jimbo nimezungumzia mkoa
Mbeya kuna mwakyembe, Arusha ni Lowasa Kilimanjaro mzee msuya
Kama mbeya mjini, Arusha mjini, kawe, Ubungo, Mikumi, Hai, Moshi mjini etc. Si kweli eeeh[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Mwigulu ni kama nembo ya singida Mkuu si rahisi kumtoa
Kila mkoa unambunge ambaye ni nembo ya mkoa fulani

Naomba unitajie Wabunge wako ambao ni Nembo ya Mikoa ya Dar es Salaam, Mara, Morogoro, Kilimanjaro, Rukwa, Tabora, Pwani na Lindi Ndugu.
 
Watu wanaombea Dkt na Waziri wa Sheria na Katiba Lameck Madelu Mwigulu Nchemba akatwe na Halmashauri Kuu ili asigombee Ubunge ili apate nafasi ya kujijenga akisubiri mpaka 2025 aje kugombea Urais ili kutimiza ndoto yake.

Watu wanatarajia watu wapya kujitokeza kuchukua Fomu na kumpa changamoto Dkt Mwigulu. Kuna ambao wameshaonesha waziwazi kuwa wanagombea akiwepo Jumbe Katala ambaye tayari kishajitangaza sana kwa kupitia shule yake ya Sekondari iliyoanzishwa hivi karibuni. Wengine ni kama Dkt. Zaipuna Yona ambaye anasafiria nyota ya mke wake ambaye kwa sasa ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ambayo inafanya vizuri kwenye soko.

Mpinzani wa siku zote wa Dkt Mwigulu Profesa Kitila Mkumbo anaonekana yupo katika hali isiyo nzuri kwani Katibu Mwenezi wa CCM amekuwa akiwatisha wanaCCM wale ambao wamepewa nafasi zingine za kiutendaji wasijaribu kwenda kugombea kuwa watakatwa tu. Habari za ndani zinadai Prof. Kitila Mkumbo anaelekea kuwa tayari hata kurudi kwenye chama chake cha Act Wazalendo ili agombee ubunge Iramba kwani tayari ana uhakika na wafuasi wa kutosha ama ndani au nje ya CCM.

Msisitizo wa wananchi wengi niliokutana nao kwa takribani majuma mawili sasa wanashauri kuwa Dkt. Mwigulu inabidi atoke kwanza baada ya kukamilisha miaka kumi ya ubunge ili arudi baadaye kumpisha hata mtu ambaye atamwandaa yeye mwenyewe. Kuna watu ambao inaonyesha Dkt. Mwigulu amekuwa na ukaribu nao ili wamuunge mkono katika harakati hizi lkn pia watu hao inaonyesha wanastahili kushika nafasi hiyo. Hawa ni pamoja na William Shila wa Ulemo, aliyekuwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani Kanali Kingu, Richard Mkumbo Mkuruenzi Sera Wizara ya fedha, Bwana Kitandu Ugula, Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Mmiliki wa Chuo cha Ualimu Singida na baadhi ya wafanyabiashara wa Singida Mjini.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Iramba kwa awamu moja na sasa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma kilimba naye anapambana kivyake na huku akimchafua Dkt. Mwigulu Nchemba kwa chinichini ili arudi bungeni mwaka huu. Juma Kilimba wanashirikiana na Jesca Kisho - Mke wa Kafulila ili kuhakikisha angalau Dkt. Mwigulu anaishia miaka kumi tu ambayo Kampeni yake (kumi ya Mwigulu yatosha) imeanza rasmi Iramba.
Mtu anayeiga kampeni kwenye mawe???
 
Mwigulu ni kama nembo ya singida Mkuu si rahisi kumtoa
Kila mkoa unambunge ambaye ni nembo ya mkoa fulani
Membe asizuiwe kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM, ili Magufuli ajipime kupitia kwake namna anavyokubalika ndani ya chama chake na pia kuonesha demokrasia kama kweli ipo huko.
 
Membe asizuiwe kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM, ili Magufuli ajipime kupitia kwake namna anavyokubalika ndani ya chama chake na pia kuonesha demokrasia kama kweli ipo huko.
Kwa hiyo watakiri kweli kuwa hawajamfukuza?
 
2025 atatokea Zenji, possibly Hussein Mwinyi. 2035 itabidi atoke magharibi ya Tanzania (Mbeya, Iringa, Kigoma, Rukwa) kama huyo Mwigulu bado atakuwa relevant labda hiyo 2035 awe PM au Waziri mwandamizi kwenye wizara nyetinyeti..

President hapana, he isn't worthy it!!
No one knows what the future holds.
 
Back
Top Bottom