LGE2024 Kampeni: Mgombea awataka raia wazidi kuzaliana ili serikali ijenge shule

LGE2024 Kampeni: Mgombea awataka raia wazidi kuzaliana ili serikali ijenge shule

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kambarage uliyopo katika halmashauri ya mji wa Njombe anayetetea nafasi hiyo kwa mara nyingine, Francis Msanga ametoa wito kwa wananchi wa mtaa huo kuongeza kasi ya kupata watoto na idadi ya wananchi iongezeke zaidi ili serikali iweze kuwapa shule ya sekondari na kata.

Msanga ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe uliofanyika kwenye mtaa huo ambapo amesema katika sekta ya elimu kwenye mtaa huo wenye watu 15,195 serikali imefanya makubwa ikiwemo kujenga shule ya msingi ya pili na kupelekea mtaa kuwa na wanafunzi zaidi ya 1,800 kwa shule za msingi huku wakiwa hawana sekondari.

Soma pia: Ubungo: Kiongozi wa ACT Wazalendo aonya wananchi kupumbazwa na mambo ya Simba na Yanga

"Kwa wingi wa wananchi hawa wanazaa sana na kuongezeka na idadi yetu mkoa wa Njombe tuna wananchi wachache na nimewambia wanawake wakazane kuzaa na kwa miaka yangu mitano hatuwezi kurudi nyuma tukawa na idadi ndogo kwa hiyo tunaomba kata kwenye mtaa wetu wa mama wakazae na shule tuzipate," amesema Msanga.

Amesema kulingana na idadi ya watu waliopo pia inapelekea wanafunzi zaidi ya 300 kumaliza kwa mwaka mmoja hivyo wanaiomba serikali kukamilisha mchakato ambao mtaa ulianzisha kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari katika eneo la Magereza ili watoto wasome karibu.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika ameahidi kushughulikia swala hilo ambapo kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari eneo la Magereza mchakato unaendelea na wanatarajia kupata shule katika eneo hilo.
1732190490220.png
Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom