Kampeni nyingi za utunzaji mazingira nchini zinazalisha fedha ambazo hazitumiki moja kwa moja kutunza mazingira

Kampeni nyingi za utunzaji mazingira nchini zinazalisha fedha ambazo hazitumiki moja kwa moja kutunza mazingira

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Zipo kampeni nyingi sana zilizowahi kufanyika na zinafanyika Nchini juu ya utunzaji wa mazingira lakini kinachofanyika ni tofauti sana.

Watu wanatumia gharama kubwa sana kuzunguka Nchini, posho nauli n.k lakini tukiangalia kwa kina tunaona fedha inayotumika kwenye kampeni hizo ni kubwa kuliko matokeo yenyewe kutokana na uwekezaji duni wa moja kwa moja kwenye mazingira.

Tujiulize ni miti mingapi imepandwa, vyanzo vingapi vya maji vimetunzwa, uoto na viumbe wangapi wapo salama. Halafu tujiulize ni kiasi gani kinatumika kwenye kampeni ili kuona uwiano wa uwekezaji wetu na matokeo yake.
 
Sisi hufanya kila kitu kwa maslahi binafsi, itokee tu mradi ulete tija ila kwa aliyeubuni alilenga kujinufaisha tu.
 
Natafakari miradi kama HADO, HASHI ya miaka hiyo ukiachilia mbali hii inayosimamiwa na Wizara ya maliasili na utalii utaona kuna mahali utakwama sana
 
Back
Top Bottom