Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema
Wednesday, 09 February 2011 22:08
Hamad Rashid![]()
Mwandishi Wetu, Dodoma
"Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.
Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.
Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.
Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara.
Cheyo huyu aliyesaidiwa nyumba yake ilipokuwa inanadiwa ...sidhani kama ataweza kuibana CCM ....ngoja tuona na tusubiri, lakini mimi naona kwake itakuwa funika kombe mwanaharamu apite hata kama wataona madudu mengi