Kampeni ya kusafisha jiji la Dar es Salaam

Kampeni ya kusafisha jiji la Dar es Salaam

"KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI";

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...
Mpaka sasa kilimo ndicho chenye faida kuliko shughuli yeyote hapa Tanzania.
Nawashangaa hawa watu wanaongangania kukaa mjini kuchuuza vibidhaa kwenye masoko mabaya kama zizi la ng'ombe.
 
Huko vijijini hakuna ishu..hao jamaa wa Karume ilikuwa haina jinsi kila walivyoambiwa watoke hapo kupisha mradi wa ujenzi wa mwendokasi wanajifanya vichwa maji...ona sasa kilichotokea tena ni mita chache tu kutoka kwa Mkuu wa mkoa. Vibaka wanaenda kuongezeka mitaani...Wito wangu kwa serikali ni kuwa wasafishe hilo eneo halafu lijengwe soko la ghorofa then wamachinga wapewe vizimba ambavyo watalipia kodi kila siku ili kuingizia mapato serikali.
Machinga complex bado halija jaa
 
Moto WA michongo huo maana mchana unaona aibu kuwaka sijawahi kuona ukiwaka mchana
 
Poleni wahanga wa kampeni hii ya kuliweka "JIJI" katika hali ya "usafi".

Tumeshuhudia masoko yaliyopo katikati ya jiji letu pendwa yakiondoka moja baada ya moja ..Tulianza na

Soko la kariakoo[emoji91]

Soko la mitumba karume [emoji91]

Wats next?

Ilala kwa wauza mitumba ?

Poleni wahanga hususani wale waliolaza mizigo yao ndani ya soko.Sidhani kama kuna mtu aliyefanikiwa kutoka hata na kiatu.

Uzi tayari
@sang'udi Njoo huku Kamanda
Hangaya anazidi kuiteketeza Sukuma Gang
 
Pale waliyopata hasara ni wafanya biashara
Ila ile mirunda na mabati siyo issue

Ova
 
Wamachinga warudi Vijijini wajikite na Kilimo.
Kiliimo ukisikie tu. Ndugu yangu ameweka pesa yake ya kustaafu huko mvua Hakuna Marvuno yameungua yote. Sasa huko ndio mnatuelekeza KUTUMALIZIA HUKO. Hata cha umwagiliaji ka kutegemea Maji ya mito .ni kazi bure . Tushukuru bwawa la steigler litawapatia watut walimao upande wa chini yake uhakika wa maji mud wote kwa kilimo cha umwagiliaji.
 
Poleni wahanga wa kampeni hii ya kuliweka "JIJI" katika hali ya "usafi".

Tumeshuhudia masoko yaliyopo katikati ya jiji letu pendwa yakiondoka moja baada ya moja ..Tulianza na

Soko la kariakoo🔥

Soko la mitumba karume 🔥

Wats next?

Ilala kwa wauza mitumba ?

Poleni wahanga hususani wale waliolaza mizigo yao ndani ya soko.Sidhani kama kuna mtu aliyefanikiwa kutoka hata na kiatu.

Uzi tayari
Shule za sekondari ziliungua moja baada ya nyingine humu JF mlikaa kimya kama vile hakuna kilichotokea, na hili kaeni kimya kwanza hamlipi kodi wala hamyasafishi masoko, uchafu ukizidi husababisha mlipuko wa moto.
 
"KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI";

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.
Asante Kwa kutuletea shairi mujarab!

Alichosema baba ni kweli. Leo hii tu nimesoma kuwa huko Kenya, mti mmoja wa Avacado huzalisha matunda yenye thamani kama $650 kwa mwaka. Avacado zinalindwa usiku na sungusungu!
 
Kiliimo ukisikie tu. Ndugu yangu ameweka pesa yake ya kustaafu huko mvua Hakuna Marvuno yameungua yote. Sasa huko ndio mnatuelekeza KUTUMALIZIA HUKO. Hata cha umwagiliaji ka kutegemea Maji ya mito .ni kazi bure . Tushukuru bwawa la steigler litawapatia watut walimao upande wa chini yake uhakika wa maji mud wote kwa kilimo cha umwagiliaji.
Kwahiyo unafikiri solution ni Nchi nzima kuja Dar kuchuuza?
 
Asante Kwa kutuletea shairi mujarab!

Alichosema baba ni kweli. Leo hii tu nimesoma kuwa huko Kenya, mti mmoja wa Avacado huzalisha matunda yenye thamani kama $650 kwa mwaka. Avacado zinalindwa usiku na sungusungu!
... yap; vijana na nguvu zao waache uvivu wa kukaa mabarabarani bila kazi wakati mapori yamejaa tele. Unakuta likijana barubaru eti kinachomweka mjini ni kuendesha bajaji au bodaboda au kuchuuza karanga barabarani na kwenye mabaa! Dah!
 
Mpaka sasa kilimo ndicho chenye faida kuliko shughuli yeyote hapa Tanzania.
Nawashangaa hawa watu wanaongangania kukaa mjini kuchuuza vibidhaa kwenye masoko mabaya kama zizi la ng'ombe.
Mkuu hlo shairi Sina uhakika Kama ulilisoma darasan au umrkutana nalo jf, ila linamaudhui zaidi ya hicho ulichokiandika, kwa ufupi tu, hao watt walilima na kupata mazao waliyauza wapi?? Walipataje yumba za matofari?? Hvyo vifaa walivipata wapi?? Walikuwa na maisha Bora je hayo maisha Bora waliayapataje??

Huenda hujaelewa ngoja nifafanue kidg, kilimo Ni uti wa mgogo wa taifa letu, isipokuwa haujawekewa mkazo kwenye bajet za kiserikali, hebu angalia benk za kilimo zote zipo mjin na pesa zake kuzipata kunamlolongo wa kudondoka mtu, Sasa Hy mkulima Kama anahitaji hicho kilimo Cha kubadili kabisa maisha yake lazima ajiweke kwenye kilimo Cha umwagiliaji, Sasa twende Sasa hao maafisa ugani wapo?! Au nao wamekuwa bank wanakaa mjin wanakwenda vijijin nakurud mjin jion?[emoji15][emoji15]

Changamoto ya kilimo Ni kubwa mno na imefanywa makusudi na watunga sera za nchi kwa kuizingazinaga Sana, yaan njia ya kufanikiwa kupitia kilimo Ni kwa mazao yenyewe na wanaofaidika si wakulima ila wale wanaofanya biashara hyo, ila mkulima anaendelea kuwa chini tu
 
Poleni wahanga wa kampeni hii ya kuliweka "JIJI" katika hali ya "usafi".

Tumeshuhudia masoko yaliyopo katikati ya jiji letu pendwa yakiondoka moja baada ya moja ..Tulianza na

Soko la kariakoo🔥

Soko la mitumba karume 🔥

Wats next?

Ilala kwa wauza mitumba ?

Poleni wahanga hususani wale waliolaza mizigo yao ndani ya soko.Sidhani kama kuna mtu aliyefanikiwa kutoka hata na kiatu.

Uzi tayari
Baada ya kuungua la karume, hayo mengine yaliyobaki watu watafukuzwa kwa nguvu kwa kigezo cha kuboresha miundombinu ili na yenyewe yasije yakaungua usiku.
Huo ndio utakuwa mwisho wa mpango mkakatu. Stay tuned ndugu wamachinga.
 
Back
Top Bottom