Kampeni ya Mama Samia Legal Aid yatarajiwa kuanza Mwanza kuanzia Februari 18 hadi 27. Mkuu wa mkoa atoa neno

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid yatarajiwa kuanza Mwanza kuanzia Februari 18 hadi 27. Mkuu wa mkoa atoa neno

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mkoa wa Mwanza unatarajia kuzindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itakayodumu kwa muda wa siku 10 kutoka Februari 18 hadi 27 mwaka huu katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema mara baada ya kuzinduliwa, msaada wa kisheria unatarajia kuendelea katika wilaya zote nane za mkoa huo.

Soma pia: Kilimanjaro: Samia Legal Aid Campaign yatatua mgogoro wa ardhi uliodumu miaka zaidi ya 30

Mtanda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni hiyo huku akiwataka wananchi wenye changamoto za kisheria kufuatilia ratiba katika wilaya zao kujua maeneo ambayo msaada wa kisheria utakuwa unatolewa.

 
Mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama mama
1739388788187.jpg
 
Hiyo kampeni inaendeshwa kutoka kwenye fungu la bajeti gani ya serikali?
 
Back
Top Bottom