benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Wizara ya Katiba na Sheria imezindua kampeni ya msaada wa kisheria kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria nchi nzima kwa miaka mitatu.
Kupitia katika kampeni hiyo wananchi wataelimishwa juu ya haki ya kulinda mila na desturi nchini, kupingana na mila potofu kutoka nje ya nchi na utoaji wa msaada wa kisheria kwa kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii.
Akizindua kampeni hiyo ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid Campaign, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Numbaro alitaja kaulimbiu ya kampeni hiyo kuwa ni:
"'Ungana na Mama Samia kupinga Ukatili, Heshimu Utu wa Mwenzako; Linda Mtoto wa Mwenzako; Tujenge nchi yenye Staha, Heshima na Amani".
Alisema kampeni hiyo itatekelezwa Zanzibar na Tanzania Bara na kwa kuzingatia mahitaji halisi ukilinganisha na ukubwa wa nchi kampeni hii itatekelez-wa kwa awamu tatu kwa muda wa miaka mitatu na kukamilika Desemba mwaka 2026.
Dk Ndumbaro alitaja mifumo itakayoshughulikiwa kuwa ni usimamizi wa mirathi na urithi, sheria ya ardhi na haki ya kumiliki mali, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala hususani kwa viongozi wa serikali za mitaa, watendaji wa kata, vijiji na wajumbe wa mabaraza ya ardhi, wazee wa kimila nawazee maarufu na viongozi wa dini.
Alisema kampeni hiyo imepewa jina la Rais Samia kutokana na jitihada zake za kuzingatia haki za binadamu, utawala wa sheria, utii wa sheria na elimu ya kikatiba na ya kisheria kwa umma.
Alisema kumekuwa na mafanikio ya kisheria katika utoaji haki kwa kuanzisha na kutambua kada ya wasaidizi wa kisheria na kuanzia mwaka 2017 mpaka mwaka huu wasaidizi 4,790 walipatiwa mafunzo na 1,073 kusailiwa na kupatiwa leseni Tanzania Bara.
Pia Zanzibar waliwapatia mafunzo wasaidizi wa kisheria 370 na 258 wakisajiliwa na kupatiwa leseni na watu milioni 3.2 wamepatiwa elimu ya sheria na haki za bi-nadamu nchini katika miezi sita huku 42,000 wakipatiwa msaada wa sheria kwa miezi sita.