The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kampeni ya Mtu ni Afya kwa sasa imeufikia mkoa wa Arusha na tarehe 27 Februari 2025 imeendelea katika Wilaya ya Longido mji wa Namanga na kata zake
lengo ikiwa ni kuwafikia wakazi wa meeneo yote kuwaeleza manufaa ya afua tisa za kampeni hiyo.
Judithi Meela ni Afisa Afya wa Wilaya ya Longido amesema Kampeni hiyo itasaidia kupambana na tatizo la lishe, masuala ya hedhi kwa akina mama ambayo yamekuwa changamoto.
"Lishe ni moja ya changamoto inayizikumba familia za kifugaji kwani muda mwingi hawafuati mlolongo mzuri wa matumizi ya chakula bora hii inapelekea kuwepo na wimbi kubwa la watu wenye utapiamlo" amesema Bi Meela
Kwa upande wake Evance Simkoko ambaye ni Afisa Afya mkuu kutoka Wizara ya Afya yeye amesema kampeni hii ina afua tisa ambazo zinatekelezwa na zinamlenga mtanzania wa hali zote
Mjumbe wa serikali ya kijiji Reketai ameshiriki katika kampeni ya Mtu ni Afya na amesema kampeni hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa hawaelewi namna ya kuishi salama na vyoo lakini wamehamasika kwa kila kaya kuwa na choo bora
Kampeni ya Mtu ni Afya ina kauli mbiu isemayo 'FANYA KWELI USIBAKI NYUMA