Kampeni ya vijana kukataa ndoa ni matokeo ya kumtenga mtoto wa kiume katika malezi

Kampeni ya vijana kukataa ndoa ni matokeo ya kumtenga mtoto wa kiume katika malezi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
1️⃣ Tumeshuhudia ongezeko la vijana wa kiume wanaokataa ndoa au kuikwepa. Hili si jambo la bahati mbaya, bali ni matokeo ya malezi yaliyomwacha mtoto wa kiume bila mwongozo wa kutosha.

2️⃣ Kwa miaka mingi, harakati za kumwinua mwanamke zilihamasisha elimu, ajira, na haki za wanawake, jambo ambalo ni jema. Lakini, kwa upande mwingine, kampeni hizi hazikutoa msukumo sawa kwa malezi ya mtoto wa kiume. Mambo yalianzia Beijing na kuona mtoto wa kike pekee anapaswa kupewa kipaumbele cha malezi.

3️⃣ MTOTO WA KIUME AMEACHWA ANAJILEA. Amefundishwa kuwa anapaswa kuwa mgumu, kupambana mwenyewe, na mara nyingi amekosa mifano mizuri ya ndoa kutoka kwa wale waliomtangulia.

4️⃣ Wavulana wengi wamekulia kwenye familia zenye mzazi mmoja, hasa mama pekee, ambaye anapambana kulea peke yake. Hili limewafanya baadhi ya wanaume wasione ndoa kama taasisi inayostahili kuheshimiwa au kutafutwa na au kuwa mfano wa maisha imara ya familia. Wanaona ndoa ni taasisi ya ngono na kuzaa, jambo wanalohisi linaweza kukamilika hata nje ya taasisi hiyo.

5️⃣ Wengine wamekulia katika mazingira ya baba asiyejali, baba aliyekimbia majukumu, au baba aliyepo lakini hayupo kiuhalisia. Hawakujifunza upendo wa kweli wa ndoa bali waliona ndoa kama mzigo au jela ya maisha.

6️⃣ Katika jamii, mtoto wa kiume amekuzwa akiambiwa "wanaume hawalii," "wanaume hawana matatizo ya kihisia," na "wanaume wanapaswa kuwa wagumu." Hii imemfanya ajitenge na mahusiano yenye hisia za dhati, ikiwa ni pamoja na ndoa.

7️⃣ Vijana wengi wa kiume sasa wanachagua kuishi peke yao, kuepuka mahusiano ya kudumu, na wengine kujiingiza kwenye maisha ya anasa bila mipango ya kuanzisha familia. Kwao, ndoa si kipaumbele tena.

8️⃣ Tunapaswa kutathmini upya mfumo wetu wa malezi. Kupambana kwa ajili ya haki za wanawake haipaswi kumaanisha kumsahau mtoto wa kiume. Lazima tuwaelekeze wavulana juu ya thamani ya familia, uongozi wa heshima, na mapenzi ya dhati.

9️⃣ Hatuwezi kuwa na jamii imara ikiwa kizazi cha sasa cha wanaume hakioni thamani ya ndoa. Tunahitaji kampeni mpya za malezi zinazomhusisha mtoto wa kiume, zikifundisha wajibu wake katika familia na jamii.

🔟 Tuanzishe mjadala: Je, malezi yanayompuuza mtoto wa kiume yamechangia kwa kiasi gani katika kizazi cha vijana wanaokataa ndoa? Tuambie maoni yako.

MY TAKE ⬇️:
Zichukuliwe jitihada za maksudi kuijenga jamii ya kiume ione umuhimu wa ndoa kwa kuwa taifa imara linaanzia kwenye taasisi ya ndoa.

CC: @Dgwajima
 
Screenshot_20250304-203214~2.jpg
 
Hizi Mada za "Kataa Ndoa" humu JF nimeanza kuzisoma Tangu Nipo Lindo Past Years Mpaka Leo Nipo Chuo Duuh.
Binafsi SijaOA Bado ila kwa Upeo Wangu Haya Mambo Ni Kumuomba MUNGU Akupe Mtu Sahihii. That's All.
Ila uoe mkuu usiwasikilize hawa jenizii wa humu
 
Back
Top Bottom