Kampeni ya vijana kukataa ndoa ni matokeo ya kumtenga mtoto wa kiume katika malezi

Kampeni ya vijana kukataa ndoa ni matokeo ya kumtenga mtoto wa kiume katika malezi

Serikali itutambue Kataa Ndoa.
Nyinyi mpango uliopo ni kuwakusanya wote kuwatandika viboko 20 kila mmoja wenu kisha kuwaonesha mke wa kuoa na kuwasimamia muoe kwa bunduki kabisa.
Hamuwezi kukataa kuwaoa wana wa kike wa Tanzania nyi nani?
 
Uhalisia kuhusu ndoa ni huu : ndoa za zamani walikuwa wakifunga ndoa wakiwa wadogo ,ule mri wa balekhe ila kwa leo ili mtu awe tayari basi awe kamaliza chuo ,miaka 22-23 na kuendelea.
Sasa gap la kuanzia miaka 18 akiwa active kweny mapenzi mpaka akijamaliza chuo kashachoka ,mambo yote anayajua hamna kipya kwake.

Mwanamke anakuwa na wanaume wengi aliotembea nao ,hata bikra kashapoteza ..Ikitokea kijana ukaoa basi jiandae kwa matatizo.

Ndoa ilikuwa na maana watu kuingia mapema mno wanapofika umri wa kubalekhe tu .​
 
Nyinyi mpango uliopo ni kuwakusanya wote kuwatandika viboko 20 kila mmoja wenu kisha kuwaonesha mke wa kuoa na kuwasimamia muoe kwa bunduki kabisa.
Hamuwezi kukataa kuwaoa wana wa kike wa Tanzania nyi nani?
ni mwendo wa kukataa ndoa hatutaki stress ,naomba tupeni elimu zaidi ili tuwaelewe maana kila siku tunasikia ugomvi baina ya wanandoa sijui amenyimwa tendo la ndoa ,sijui mke amemcheat mumeo waziwazi na hii yote inapelekea magonjwa ya akili kwa sababu ya mbilinge zote kam stress na ugomvi usioishi ,njoeni na hoja itakayotulinda huko ndoani
 
Akili sana zipi hizi za kudownload movie au wameanza kutengeneza vitu vinaenda angani?

Taratibu Mkuu😲😲
Screenshot_20250304-230326_1741118668970.jpg
 
ni mwendo wa kukataa ndoa hatutaki stress ,naomba tupeni elimu zaidi ili tuwaelewe maana kila siku tunasikia ugomvi baina ya wanandoa sijui amenyimwa tendo la ndoa ,sijui mke amemcheat mumeo waziwazi na hii yote inapelekea magonjwa ya akili kwa sababu ya mbilinge zote kam stress na ugomvi usioishi ,njoeni na hoja itakayotulinda huko ndoani
Kwa mtazamo wako unadhani ipi ni njia sahihi ya kulea watoto, kama hamtaki ndoa
 
1️⃣ Tumeshuhudia ongezeko la vijana wa kiume wanaokataa ndoa au kuikwepa. Hili si jambo la bahati mbaya, bali ni matokeo ya malezi yaliyomwacha mtoto wa kiume bila mwongozo wa kutosha.

2️⃣ Kwa miaka mingi, harakati za kumwinua mwanamke zilihamasisha elimu, ajira, na haki za wanawake, jambo ambalo ni jema. Lakini, kwa upande mwingine, kampeni hizi hazikutoa msukumo sawa kwa malezi ya mtoto wa kiume. Mambo yalianzia Beijing na kuona mtoto wa kike pekee anapaswa kupewa kipaumbele cha malezi.

3️⃣ MTOTO WA KIUME AMEACHWA ANAJILEA. Amefundishwa kuwa anapaswa kuwa mgumu, kupambana mwenyewe, na mara nyingi amekosa mifano mizuri ya ndoa kutoka kwa wale waliomtangulia.

4️⃣ Wavulana wengi wamekulia kwenye familia zenye mzazi mmoja, hasa mama pekee, ambaye anapambana kulea peke yake. Hili limewafanya baadhi ya wanaume wasione ndoa kama taasisi inayostahili kuheshimiwa au kutafutwa na au kuwa mfano wa maisha imara ya familia. Wanaona ndoa ni taasisi ya ngono na kuzaa, jambo wanalohisi linaweza kukamilika hata nje ya taasisi hiyo.

5️⃣ Wengine wamekulia katika mazingira ya baba asiyejali, baba aliyekimbia majukumu, au baba aliyepo lakini hayupo kiuhalisia. Hawakujifunza upendo wa kweli wa ndoa bali waliona ndoa kama mzigo au jela ya maisha.

6️⃣ Katika jamii, mtoto wa kiume amekuzwa akiambiwa "wanaume hawalii," "wanaume hawana matatizo ya kihisia," na "wanaume wanapaswa kuwa wagumu." Hii imemfanya ajitenge na mahusiano yenye hisia za dhati, ikiwa ni pamoja na ndoa.

7️⃣ Vijana wengi wa kiume sasa wanachagua kuishi peke yao, kuepuka mahusiano ya kudumu, na wengine kujiingiza kwenye maisha ya anasa bila mipango ya kuanzisha familia. Kwao, ndoa si kipaumbele tena.

8️⃣ Tunapaswa kutathmini upya mfumo wetu wa malezi. Kupambana kwa ajili ya haki za wanawake haipaswi kumaanisha kumsahau mtoto wa kiume. Lazima tuwaelekeze wavulana juu ya thamani ya familia, uongozi wa heshima, na mapenzi ya dhati.

9️⃣ Hatuwezi kuwa na jamii imara ikiwa kizazi cha sasa cha wanaume hakioni thamani ya ndoa. Tunahitaji kampeni mpya za malezi zinazomhusisha mtoto wa kiume, zikifundisha wajibu wake katika familia na jamii.

🔟 Tuanzishe mjadala: Je, malezi yanayompuuza mtoto wa kiume yamechangia kwa kiasi gani katika kizazi cha vijana wanaokataa ndoa? Tuambie maoni yako.

MY TAKE ⬇️:
Zichukuliwe jitihada za maksudi kuijenga jamii ya kiume ione umuhimu wa ndoa kwa kuwa taifa imara linaanzia kwenye taasisi ya ndoa.

CC: @Dgwajima
Mengi uliyoyasema ni kweli kabisa, lakini kuna mabinti siku hizi unamsikia kwa kujiamini kabisa na akiwa na akili timamu anasema yeye anataka kuzaa tu alee watoto wake,hataki kuolewa....... nadhani kwenye malezi bado kuna kitu hakiko sawa,baada ya miaka mitano ijayo naona mambo yatakuwa magumu zaidi
 
Tunalichukulia hili suala kiutani ila ukweli ni kwamba madogo hili litawatesa sana miaka 10 tu ijayo
 
Ukweli ni kwamba hizi kelele ni za humu Kwenye mitandao ya kijamii huku mtaani watu wanafunga ndoa kila siku.
Wanafunga ndoa ila baada ya siku chache wanakuwa awana ndoa tena ....sasa hivi ndoa tuna hesabu miaka 10 mkivuka hapo mkiwa ndani ya ndoa basi mnaweza kufika salama vingi nevyo ndoa nyingi zinavunjika ndani ya miaka 4
 
Kwa mtazamo wako unadhani ipi ni njia sahihi ya kulea watoto, kama hamtaki ndoa
jibuni hoja kwanza ninyi kam wazazi mnaotaka tuoe maana unakuta mtu anataka kuoa baada y kumpeleka msichana wa watu nyumbn wazazi wanamkataa so hapo unategemea nini
 
Back
Top Bottom