SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Kila mara naona matangazo yanatolewa kufanya kampeni ya kuchunguza kansa ya shingo ya kizazi na ya matiti kwa wanawake, lakini sijasikia tangazo la kampeni yoyote kusaidia wanaume kuchunguza kansa ya tezidume.
Kiongozi mmoja wa juu sana mstaafu hapa nchini alipatwa na tatizo la tezidume akapelekwa Marekani kwa uchunguzi.Nikawaza: Ahaa, kwa kuwa huyu mkubwa sana kapata hili tatizo linalosumbua wanaume wengi bila shaka ataanzisha taasisi/kitengo cha uhamasishaji ufahamu na matibabu ya kansa ya tezidume.Mheshimiwa huyo akageuka akaanzisha taasisi tofauti kabisa.
Maelfu ya wanaume hapa nchini wanaugua kimyakimya matatizo ya tezi dume na mwishowe kuugua kansa bila wao au jamaa zao kufahamu nini kilimwua mpendwa wao.Wanaishia kusema tu ni uchawi.
Kwa upande wa wanawake, MEWATA inafanya kazi nzuri sana kuwaamsha wanawake kutambua na kuwahi kutibu kansa za matiti na shingo ya kizazi.Sasa hivi niandikapo thread hii ipo kampeni inaandaliwa na MEWATA (Medical Women Asociation of Tanzania mkoani Njombe kuchunguza kansa za kina mama.
Hakuna anayejali kansa za wababa(Prostate Cancer?)
Madaktari wa kiume mko wapi?Au kansa za wababa sio ishu kwenu?