Elections 2010 kampeni za kupiga magoti

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
nimeona picha mbili za wagombea wakiwa wamepiga magoti katika matukio tofauti ya kampeni kule jamii photos kwa kweli hiki ni kitendo kibaya yaani sitaki kuamini mgombea anabembeleza apewe kazi ya kuwatumikia wananchi kiasi hiko mpaka anafikia kuwapigia magoti, kwani ameshindwa kuongea nao tuu na wakamwelewa, hii sasa ni kutafuta kuchaguliwa kwa kuonewa huruma badala ya kile unachokisema kwenye kampeni zako. wananchi wa Poland hawakumchagua mgombea uraisi amabaye ni pacha wa raisi aliyepita ambaye kufariki kwake ndio kulipeleka kufanyika kwa uchaguzi huo. wangeweza kumchagua tuu kwa kumuonea huruma na kama kifuta machozi kwa kuondokewa na kaka yake. sipendi tufikie hatua ya kuchagua watu kwa kuwaonea huruma kwa jinsi wanavyobembeleza mpaka kupiga maogoti. kabla sijasahau, sipendi tabia ya mgombea kulia anapokuwa ameshindwa kwenye uchaguzi, hivi siasa au uongozi ni ajira?
 
Sasa si ungeweka hizo picha hapa kuongeza mashiko ya thread yako?
Lakini kupiga magoti ni tisa, kumi ni pale JK alipokaa chini kwenye vumbi kuomba kura ya mama mlemavu huko Iringa!
 
Ni wagombea wa CCM ambao wamefilisika kisiasa ambao ndiyo huomba kura za kinafiki kwa kupiga magoti lakini dawa yao siyo kulalamika ila kuwanyimwa kura tu. Hapo watashika adabu moja kwa zote wakielewa ya kuwa mwaka huu hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Myahudi anampiga mabomu mpalestina,kwa vile mpalestina huna ndege za kivita yeye anmrushia hata mawe tu kuonesha hasira zake.

Vita ni vita tu ,mtu unapopigana naye akikupiga utaweza kumuuma hata na meno ili mradi tu

You know what i am saying

Siasa ni vita hasa uchaguzi unapokaribia

Zote ni strategies hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…