JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
nimeona picha mbili za wagombea wakiwa wamepiga magoti katika matukio tofauti ya kampeni kule jamii photos kwa kweli hiki ni kitendo kibaya yaani sitaki kuamini mgombea anabembeleza apewe kazi ya kuwatumikia wananchi kiasi hiko mpaka anafikia kuwapigia magoti, kwani ameshindwa kuongea nao tuu na wakamwelewa, hii sasa ni kutafuta kuchaguliwa kwa kuonewa huruma badala ya kile unachokisema kwenye kampeni zako. wananchi wa Poland hawakumchagua mgombea uraisi amabaye ni pacha wa raisi aliyepita ambaye kufariki kwake ndio kulipeleka kufanyika kwa uchaguzi huo. wangeweza kumchagua tuu kwa kumuonea huruma na kama kifuta machozi kwa kuondokewa na kaka yake. sipendi tufikie hatua ya kuchagua watu kwa kuwaonea huruma kwa jinsi wanavyobembeleza mpaka kupiga maogoti. kabla sijasahau, sipendi tabia ya mgombea kulia anapokuwa ameshindwa kwenye uchaguzi, hivi siasa au uongozi ni ajira?