Uchaguzi 2020 Kampeni za mwaka huu kwa upande wa Chama Tawala zitachosha sana masikio

Uchaguzi 2020 Kampeni za mwaka huu kwa upande wa Chama Tawala zitachosha sana masikio

Louis II

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
3,030
Reaction score
4,647
Sina hakika kama kutakuwa msamiati mpya. Kuna maneno yamekuwa adimu sana kuyasikia kwenye zile insha za kusifu na kuabudu.

Maneno haya yamekuwa adimu kwakweli ajira, ongezeko la mishahara na upandishwaji wa madaraja kwa watumishi, usawa, umoja wa kitaifa, usawa nk. Bila shaka hatutayasikia yakipambwa wakati wa kampeni maana hayakutekelezwa (Aibu).

Tutarajie maneno kama ndege, flyover, Stieglers Gorge, ujenzi wa mabarabara, elimu bure na umeme wa REA. Haya maneno yanachosha sana na yatafanya kampeni zipooze/ziboe. Masikio yatachoka sana.

UPDATE
Kuna mdau kanikumbusha na zile milioni 50 kila kijiji hatutasikia mbwembwe za kujinadi nazo tena.
 
Ilani ya mwaka 2015 walisema hayo
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kanuni bora za kilimo kwa kuongeza idadi ya maafisa ugani kutoka 9,558 waliopo sasa hadi kufikia 15,082 mwaka 2020;
 
Ilani ya mwaka 2015 walisema hayo
Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kanuni bora za kilimo kwa kuongeza idadi ya maafisa ugani kutoka 9,558 waliopo sasa hadi kufikia 15,082 mwaka 2020;
Wametekeleza?
 
Nilishasahau hii ngonjera..Kweli CCM wana madeni mengi sana kwa Watanzania.
Kuna akina mama walitapeliwa na wajanja kwamba waandike majina yao na kutoa 50000 kila mmoja ili wasajiliwe katika vikundi halafu millioni hamsini zikija wao watapata millioni kumi kwa awamu ya kwanza. Wale jamaa walikula hela mpaka walijipatia matunda kimasihara.

Swali: Hivi kuna vijiji vingapi na mitaa mingapi nchini?
Bajeti ingetosha?
Jumla=50,000,000*(idadi ya vijiji na mitaa)
 
Akilindogosana,
m50 zitamtesa sana Magu mwaka huu. Sijui ataambia nini watu. Just imagine unamwambia mtu wa Sikonge bush huko eti umenunua ndege au unajenga reli ya SGR.
 
m50 zitamtesa sana Magu mwaka huu. Sijui ataambia nini watu. Just imagine unamwambia mtu wa Sikonge bush huko eti umenunua ndege au unajenga reli ya SGR.
Mtanzania hana kumbukumbu nzuri. 2020 tayari ameshashinda kwa kishindo kikubwa hata uchaguzi ukiwa wa huru na haki. Sera ya elimu bure kwa huku mikoani wananchi huwambii kitu juu ya CCM, wananchi watampigia kura mpaka watu mtashangaa.
 
Wakulima wa korosho hawataki Hata kuisikia ccm

Watumishi wa umma hawana muda nayo imeshawanyoosha

Wafanya biashara hawana usemi wana izoom tuu

Mambo Mengi hawana pakushika
 
Muda ni mwamuzi mzuri sana.
 
Wakulima wa korosho hawataki Hata kuisikia ccm

Watumishi wa umma hawana muda nayo imeshawanyoosha

Wafanya biashara hawana usemi wana izoom tuu

Mambo Mengi hawana pakushika
Duuh huko kwenye korosho ndio kalikoroga kabisaa.
 
Wametekeleza?
Hawajatekeleza wakija na sera zao hizo kama uchaguzi ungekuwa huru na haki mchana kweupe wangeshindwa. Maana wapinzani wakija na sera kwa wapiga kura kuwa mnataka maendeleo ya vitu au mnataka maendeleo ya vitu yaende sambamba na maendeleo ya watu
 
Thubutu! Ni afadhali hata enzi za ada kuliko kipindi hiki cha elimu bure; yaani kuna utitiri wa michango yenye kukera sijapata kuona.

Utaambiwa ulipe 50,000 ya taaluma, 12,000 ya ulinzi, 15,000 ujenzi wa darasa, 5000 ujenzi wa matundu ya vyoo, 30,000 kwa ajili ya uji kwa mtoto wa drs la awali n.k.

Kiujumla hii elimu bure ni majanga tu.
Mtanzania hana kumbukumbu nzuri. 2020 tayari ameshashinda kwa kishindo kikubwa hata uchaguzi ukiwa wa huru na haki. Sera ya elimu bure kwa huku mikoani wananchi huwambii kitu juu ya CCM, wananchi watampigia kura mpaka watu mtashangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ben Bella,
Nilifika kijijini kwa Mjomba wangu akaniambia kuwa anatakiwa atoe Sh. 40,000/= za chakula cha mtoto na ana watoto wawili means alipaswa kutoa 80000/=……Waliposema elimu bure walipaswa watoe uchanganuzi na ufafanuzi . In short elimu sio bure kama wanavyojinadi.
 
Hawajatekeleza wakija na sera zao hizo kama uchaguzi ungekuwa huru na haki mchana kweupe wangeshindwa. Maana wapinzani wakija na sera kwa wapiga kura kuwa mnataka maendeleo ya vitu au mnataka maendeleo ya vitu yaende sambamba na maendeleo ya watu
Ila mwaka huu sipati picha.
 
Back
Top Bottom