CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Ni bahati mbaya mikutano ya CHADEMA na ACT wanaoulizwa maswali ni Wananchi waliokuja kuwasikiliza badala ya wananchi kuwauliza wao maswali. Kwa kuwa siku bado ningefurahi kama kuna atakayewauliza wagombea wakuu wa CHADEMA na ACT haya maswali yangu. Au tufanye mdahalo nao? Maswali yangu ni haya:
1. Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu ushoga? Ni kweli wakipata nafasi watabadili sheria ili kila mtu awe na haki ya kutumia mwili wake atakavyo? Ni kweli ushoga ni moja ya haki za binadamu?
2. CHADEMA na ACT watuambie ni kweli wakipata nafasi wataacha kutuletea vitu na badala yake watatuletea nini?
3. CHADEMA na ACT watuambie kwa kuwa wanadai serikali imefanya makosa kuleta vitu wakipata nafasi wataving'oa au kuviharibu vitu?
4. ACT watuambie ni kweli wakipata nafasi wataruhusu wanafunzi wajawazito wachanganyike na wasio wajawazito darasa na bweni moja?
5. ACT na CHADEMA watueleze watazifanyeje ndege za ATCL? Wataziuza? Watazikodisha? Wataacha zioze? Hawatanunua tena ndege wakipata nafasi? Taifa litakuwa halina shirika la ndege chini ya utawala wao?
6. CHADEMA, ACT, CUF, NCCR watueleze watakavyounda tume mpya ya uchaguzi ambayo kwa mtazamo wao itakuwa huru 100%? Nani watakuwa wajumbe na watapatikanaje?
7. Kwa kuwa Bwawa la Nyerere (Stieglers) ni la umuhimu wa kipekee kwa Taifa na Kwa kuwa wao wanalipinga je wakishika madaraka watalivunja? Wataacha lioze?
8. CHADEMA watuthibitishie utawala wa majimbo ni suala lipo kwenye sera yao? Watagawaje hayo majimbo? Wataweka tahadhari zipi ili tusitumbukie kwenye ukabila au baadhi ya maeneo kuachwa nyuma kimaendeleo? Wataweka tahadhari zipi ili tusitumbukie kwenye mifarakano kama Nigeria?
9. Kwa kuwa CHADEMA wamediriki kufukuza chombo cha habari ambacho kwa maoni yao kilikuwa hakiwafurahisi watueleze ikiwa watapata madaraka vyombo ambavyo havitawafurahisha vitalindwa kivipi?
10. CHADEMA na ACT watueleze msimamo wao kuhusu muungano kwa kuwa wagombea wao wamejikita katika kuupinga muungano. Je muungano utakuwa salama chini ya utawala wao? Watafanya nini usivunjike?
Ikiwa watashindwa kujibu au kufafanua tumia kura yako kwa busara tarehe 28/10.