joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Sasa hivi ni takriban mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika 28th October, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi sana kusikiliza sera za wagombea wa nafasi mbalimbali.
Jambo la kufurahisha na ambalo tungeomba majirani wetu kuiga Tanzania ni hili la amani na utulivu unaokuwepo katika mikutano ya wagombea mbalimbali, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyepigwa na polisi au wanachama wa vyama vya upinzani kushambuliana kwa aina yoyote ile, hii ndio maana halisi ya demokrasia, amani na utulivu.