Kampeni za uchaguzi Tanzania, fundisho kwa Kenya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Sasa hivi ni takriban mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika 28th October, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi sana kusikiliza sera za wagombea wa nafasi mbalimbali.

Jambo la kufurahisha na ambalo tungeomba majirani wetu kuiga Tanzania ni hili la amani na utulivu unaokuwepo katika mikutano ya wagombea mbalimbali, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyepigwa na polisi au wanachama wa vyama vya upinzani kushambuliana kwa aina yoyote ile, hii ndio maana halisi ya demokrasia, amani na utulivu.
 
Maana ya demokrasia ni pamoja na uchaguzi ambao ni huru na wa haki. Demokrasia sio kuchagua chagua vipengele fulani na kupuuza vingine ambavyo ni nyeti zaidi. Vipi kuhusu tume ya uchaguzi, ni ile ile ambayo ilifanya maigizo ya ajabu ajabu uchaguzi uliopita? Wanahabari nao wanafanya haki kwa wagombea wote na vyama vyote kwa kufanya 'balanced coverage' ya kampeni? TBCCM inatoa muongozo na mfano mzuri kwa wanahabari wenzao, au ipo chini ya kisigino cha chama tawala? Wafanyakazi wa umma wapo huru kujihusisha na kampeni za vyama wanavyovitaka wao au wamebanwa na 'muajiri' wao? Nina maswali kibao.
 
An opposition leader in Kenya has never been shot 16 times during the campaigns. Na mkimaliza campaigns zenu ambieni Magufuli asisahau kurudisha hile chopper alikodi kutoka Kenya.
 
"hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyepigwa na polisi au wanachama wa vyama vya upinzani kushambuliana kwa aina yoyote ile, hii ndio maana halisi ya demokrasia, amani na utulivu"

Boss una hakika na hilo? Ngoja nikukumbushe haya mawili japo tujipongeze tumejitahidi sana ila CCM,NEC na wakurugenzi wanataka kutuvurugia.
[emoji117]Mwanachama wa NCCR mageuzi alikatwa sikio vunjo
[emoji117]Wahuni wa CCM walimtupia mawe Mh Rais mtarajiwa TAL
 
Ninakumbuka hadi leo tume ya uchaguzi Kenya imekataa kufungua servers zake zikaguliwe kama mahakama ilivyoamuru, NASA ilisema tume ibadilishwe ndio warudi katika uchaguzi wa marudio kwasababu haikua huru lakini tume ilibaki ileile hadi leo [emoji23][emoji23][emoji23]

Kenya hata uhuru wa kukusanyika siku hizi haupo
Any way, muhimu hapa ni kipengele cha kampeni zenye utulivu na amani, kama ni Kenya hadi sasa sio chini ya watu 30 wangekua wameshapoteza maisha. Jifunzeni kufanya kampeni na uchaguzi bila kumwaga damu.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Tuwekee ushahidi kaka tuone

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu chek hii
Your browser is not able to display this video.
 
Tanzania nchi ya mfano. Kenya wanatuzidi kwenye udalali tu, wanachukua parachichi njombe wakiuza wanasema zimetoka kenya. Tanzanite Magufuri kawakomesha. Dhahabu pia wanaugulia maumivu tu
Your browser is not able to display this video.
 
An opposition leader in Kenya has never been shot 16 times during the campaigns. Na mkimaliza campaigns zenu ambieni Magufuli asisahau kurudisha hile chopper alikodi kutoka Kenya.
Was it during campaign or parliament sessions?, more than 50 prominent politicians in Kenya were killed through political assassinations, non in Tanzanian history has been assassinated.

Usijaribu kupindisha ukweli, kitendo cha kampeni za Tanzania kufanyika kwa amani, ni funzo kwa Kenya na Uganda.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
An opposition leader in Kenya has never been shot 16 times during the campaigns. Na mkimaliza campaigns zenu ambieni Magufuli asisahau kurudisha hile chopper alikodi kutoka Kenya.

It was not during campaigns.
And at least haikuwa kwa sababu ya ukabila.
 
Wafanyakazi wa umma wajihusishe na siasa? Una matatizo? Yaani madaktari na wenyewe wawe na bendera za kichama huko wodini? Maadili ya kazi hayawaruhusu kuonesha mirengo yao ya kisiasa sababu kazi sio siasa ni taaluma.
 
Wanatapatapa baada ya kuona tunafanya kampeni za amani na ustasrabu, ingekuwa kwao sasa hivi Nairobi ingekuwa Empty, kila mtu amerudi kijijini kwenye kabila Lake kuogopa kushambuliwa na kabila lingine hapo Nairobi.
 
Ushahidi huu apa. Amani sio? Mnafiki mkubwa wewe!
Hahahaha, jinga wewe kabisa, huyu alipigwa kwa misingi ya kisiasa au ni vijana walevi wanapigana mtaani?. Weka ushahidi kama hili linahusiana na siasa, unadhani kwasababu ni kipindi cha kampeni basi visa vya watu kupigana na kuchinjana mtaani vitakuwa havipo?, stop your stupidity.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…