Kampeni za urais USA zimetumia Shilingi Trillioni 39.7

Kampeni za urais USA zimetumia Shilingi Trillioni 39.7

Ukijaribu kubadilisha uchumi wa Marekani wa dola trilion 27 katika pesa zetu za madafu ndio utajua wako mbali kiasi gani

Kweli mkuu. Wale wapo mbali Sana. Sisi bado Sana kiwafikia.
 
Ufadhiri uko wazi na Kamala alipewa mchango mkubwa zaidi. Na kuna kampuni zilichangia wote, na kila mgombea anaweza omba kuchangiwa kwa yeyote ila sharti hela unayopewa useme ni kiasi gani na imetoka kwa nani.

Mfano Trump sera zake ni kupiga kodi kubwa magari yanayozalishwa nje ya Marekani, tiyari makampuni ya magari Marekani kama Ford yanaona yatafanikiwa zaidi Trump akiwa Marekani hivyo yanashawishika kumchangia ili aendeleze kampeni zake na ashawishi raia wampe kura.

Wakati kwa kampuni za kuuza silaha zinaona Trump hataki kutoa misaada ya silaha na kupiganisha vita hivyo hazitauza kwenye utawala wake. Zinashawishika kumchangia Kamala.

Kweli kabisa mkuu.
 
Factor in total population ya hizi nchi mbili.
Ujerumani inatumia umeme karibia sawa na Africa nzima kwa mwaka, Ujerumania ina watu milioni 85, Africa watu bilioni 1.4. Marekani inatumia umeme mara zisizipimika dhidi ya Africa nzima wakati ina raia milioni 350.
 
Ujerumani inatumia umeme karibia sawa na Africa nzima kwa mwaka, Ujerumania ina watu milioni 85, Africa watu bilioni 1.4. Marekani inatumia umeme mara zisizipimika dhidi ya Africa nzima wakati ina raia milioni 350.
Pale alikuwa analinganisha Tz na Marekan ndo ikaja hyo 240 years.
Ni kweli bado wametuacha mbali ila siyo 240 years mazee.
 
Sidhani Kama wanalipwa. Ni utaratibu wa kawaida kuchangia wagombea urais.
Katika ubepari no any thing for nothing......sema tu hujui wanafaidika je, ila wana faidika katika sera za chama pamoja na kupewa support ya serikali katika kupanua miradi yao nje ya nchi yao.
 
Pale alikuwa analinganisha Tz na Marekan ndo ikaja hyo 240 years.
Ni kweli bado wametuacha mbali ila siyo 240 years mazee.
Inawezekana, jimbo dogo kabisa la Marekani la Rhode Island lenye ukubwa karibia sawa na Dar es Salaam linatumia umeme karibia sawa na Tanzania nzima.
 
Mkuu, hata ukigeua (factor) kwa idadi ya watu, bado miaka ni mingi mno. Watu 345M kwa 60M, huo ni uwiano wa 6:1. Maana yake, itakuwa sasa miaka 240/6 = 40!!!
Watu wengi hawaelewei kwamba sisi bado ni nchi rural sana🤣, huwa nacheka sana ninapoona watawala wakitaja kufanikisha megawatts 2000 kwa mbwembwe nyingi sana na madoido miaka hii,
 
Kampeni za Uchina zina gharimu fedha kiasi gani ?
 
Kampeni za urais nchini marekani zimetumia kiasi Cha Dollar Bilioni 15.9 ambazo ni sawa na shilingi Trillioni 39.7 za kitanzania. Kwa maana nyingine ni kwamba pesa zilizotumika kwenye kampeni za urais ni nyingi kiasi Cha kukaribia Bajeti ya mwaka ya Tanzania. Kwakweli Marekani ipo mbali Sana kiuchumi, Kama kiasi hicho ndicho linatumika na wagombea wa urais pekee. Bado counties, representatives, senetors na Governors.

Source: Econonist
Hivi unajua ndani ya Marekani Moja Kuna Tanzania ngapi?
 
Back
Top Bottom