Kampuni bora katika soko la hisa la Dar es Salaam, 2022

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Hizi ndiyo kampuni 5 bora (zilizo orodheshwa katika Soko la hisa DSE) zilizo fanya vizuri kwa mwaka 2022...

5.TCC - Tanzania cigarette company
Iliweza kujipatia faida ya tsh.billion 69,ambazo imeisaidia kuwa Earning per share ya pili kwa ukubwa.
Lakini pia imeongoza kwa uwekezaji wa faida yake katika maendeleo ya Kampuni

4.CRDB BANK
Benki ya pili kwa kutengeneza faida kwa mwaka 2022 (Billion 350).
Lakini ndiyo kampuni iliyotoa asilimia kubwa ya gawio kwa kila hisa,12%...

3.TBL -Tanzania Breweries limited
Ilitengeneza faida ya zaidi ya billion 150...
Huku ikiwa na dhamana ya kutosha ya kulipa madeni ya mda mfupi na madeni ya mda mrefu...yaaani,TBL kufirisika ni ndogo.
Na pia inatoa gawio kila mwaka...

2.DSE = DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
Usishangae, soko la hisa linajiendesha kama kampuni. Lina hazina ya kutosha ya hela 87% kuzidi madeni yake. Lilitoa gawio 6.8% zaidi ya uwekezaji kwa kila hisa.

1 .TWIGA
Hili ndiyo kampuni bora kwa mwaka 2022 kwani.
  • la-la pili kwa kiwango cha gawio 11%
  • Thamani ya kampuni katika soko inaendana vizuri na thamani ya Mali zake.
  • Inawekeza vizuri faida yake katika maendeleo ya ukuaji wa Kampuni....ndiyo maana imeinunua kampuni yenzake ya Seruji SIMBA CEMENT.
Uchambuzi Wangu umezingatia vipimo vya financial ratios za P.E,EPS,ROE,DIVIDENT RATE na PBR...

Orodha hiyo inaweza ikatumika kumsaidia mtu kujua kampuni zipi za kuzipa jicho wakati wa kutaka kuwekeza.

Karibuni kwa maoni...
 
TCC inashangaza sana kila siku watumiaji wa sigara wanazidi kupungua ila wao wanazidi kuongeza faida.
Au wanadili zaidi na exportation ya tumbaku?
Ilizalisha sigara billion 9...katika sigara billion 5 zilitumika nchini na billioni 4 ziliuzwa katika nchi za SADC....
 
Hizi ndiyo kampuni 5 bora (zilizo orodheshwa katika Soko la hisa DSE) zilizo fanya vizuri kwa mwaka 2022...

5.TCC - Tanzania cigarette company
Iliweza kujipatia faida ya tsh.billion 69,ambazo imeisaidia kuwa Earning per share ya pili kwa ukubwa.
Lakini pia imeongoza kwa uwekezaji wa faida yake katika maendeleo ya Kampuni

4.CRDB BANK
Benki ya pili kwa kutengeneza faida kwa mwaka 2022 (Billion 350).
Lakini ndiyo kampuni iliyotoa asilimia kubwa ya gawio kwa kila hisa,12%...

3.TBL -Tanzania Breweries limited
Ilitengeneza faida ya zaidi ya billion 150...
Huku ikiwa na dhamana ya kutosha ya kulipa madeni ya mda mfupi na madeni ya mda mrefu...yaaani,TBL kufirisika ni ndogo.
Na pia inatoa gawio kila mwaka...

2.DSE = DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
Usishangae, soko la hisa linajiendesha kama kampuni. Lina hazina ya kutosha ya hela 87% kuzidi madeni yake. Lilitoa gawio 6.8% zaidi ya uwekezaji kwa kila hisa.

1 .TWIGA
Hili ndiyo kampuni bora kwa mwaka 2022 kwani.
  • la-la pili kwa kiwango cha gawio 11%
  • Thamani ya kampuni katika soko inaendana vizuri na thamani ya Mali zake.
  • Inawekeza vizuri faida yake katika maendeleo ya ukuaji wa Kampuni....ndiyo maana imeinunua kampuni yenzake ya Seruji SIMBA CEMENT.
Uchambuzi Wangu umezingatia vipimo vya financial ratios za P.E,EPS,ROE,DIVIDENT RATE na PBR...

Orodha hiyo inaweza ikatumika kumsaidia mtu kujua kampuni zipi za kuzipa jicho wakati wa kutaka kuwekeza.

Karibuni kwa maoni...
Hivi twiga ilifanikisha kuinunua Simba Cement
 
Ilizalisha sigara billion 9...katika sigara billion 5 zilitumika nchini na billioni 4 ziliuzwa katika nchi za SADC....
Kudadeki sigara walizozalisha ni nyingi kuliko idadi ya binadamu duniani🤣🤣

Kama sigara bil 5 zilitumika nchini huo ni wastani wa sigara 145 kwa kila Mtanzania. Hatari sana kawa kweli
 
Utt ipo upande upi? Naona uhamasishaji wa watu ni mwingi
UTT siyo kampuni bali ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja...
  • Inakusanya pesa
  • inaikopesha serikali kupitia hati fungani za mda mrefu,miaka 10/15 au 20
  • pia inamiliki hisa za makampuni kwa mfano ina miliki hisa 0.6% katika benki ya NMB
  • Nafkiri serikali imeisajili hivyo ili kuepuka kuiweka katika makato ya kodi...kwa maana Faida yako haikatwi kodi.
 
Ahsante sasa kwa wanaoweka huko hela sisi watu wa hali ya chini, milioni moja inatosha kumpa faida gani kwa mwaka.....
Kwa elimu ndogo niliyopewa naona kama ndio hesabu za kuweka mil 200 kupata faida mil 4.
 
Back
Top Bottom