hata kampuni za long distance za dar ziko na kunguni
Habari wadau,
Nipo njiani nasafiri kuelekea nyumbani kwenye msiba na nimepanda gari la Mohamed trans linalofanya safari za Bukoba-Dar.
Kwakweli huduma za magari haya yaliyowahi kupata sifa kedekede kwa huduma nzuri kipindi cha nyuma ni mbaya sana.
Kwanza gari ni chafu sana kwa ndani na inaonesha uchafu huu ni wa siku mbili zimepita. Mbaya zaidi gari lina kunguni hatari na kila abiria amelalamikia jambo hili ila wahudumu wa gari hili hawana maneno ya staha kwa abiria.
Binafsi nimekereka sana na suala hilI na nilipojaribu kumwambia muhudumu amejifanya kuwa mkali nami nikampandishia basi hapajatosha.
Imagine kunguni wanaonekana kwenye mwanga huu sasa sijui ikifika usiku itakuwaje maana magari ya Bukoba ni ya kulala Kahama na kumalizia safari kesho yake.
Nimekereka sana na sipendi mtu mwingine akereke kama.
Hii kampuni imebaki jina tu lakini huduma mbovu sana sijapata kuona.
Kilichonikera ni gari kuwa na kunguni,haiwezekani ulipe nauli 60,000/= alafu upewe huduma kama ng'ombe wanasafirishwa kwenda mnadani.
Asanteni na mniombee nifike salama
Attached Files:
Hatari: Abiria wa Bukoba msipande magari ya kampuni ya Mohamed Trans