Kampuni nyingi hazina mifumo imara kukabiliana na ongezeko la watumiaji

Kampuni nyingi hazina mifumo imara kukabiliana na ongezeko la watumiaji

mangiTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,820
Reaction score
3,062
Habari wakuu, poleni na majukumu pia.

Kuna Uzi alileta mdau mmoja kulalamikia mfumo wa TRA kuwa ifikapo muda wa kufile return Huwa unasumbua na kuchukua muda mwingi kupokea (mfumo kupakia data) hivyo huleta usumbufu kwa watumiaji

Hivi pia nmeona makampuni kadhaa nitatolea mfano katika makampuni ya ving'amuzi ambacho nimeona

Mfano Azam kwa watumiaji wa visimbuzi ikitokea tukio la mpira hasa timu kubwa kama yanga na Simba zikicheza basi mifumo Yao ya kulipia au usajili husua sua ukiacha kulipia basi Kuna kero ya usajili hasa kwa wanaojiunga kwa mara ya kwanza.

Hivyo hivyo nimeliona Jana la DStv limekuja swala la world cup kuanzia Jana Kuna changamoto ya wateja wapya kujiunga na DStv(usajili) mwanzo ilikuwa wakala au fundi anaweza kupiga simu akasajiliwa ila Sasa simu ukipiga kuwapata ngumu halafu mawakala nao wanawategemea HQ wasajili ila wakala anaweza kukaa na details Hadi 5hrs mteja hajasajiliwa kitu ambacho huleta kero wadau mmekutana na hizi changamoto?
 
Back
Top Bottom