Kampuni tajiri duniani zinavyokamua nchi masikini

Joined
Feb 13, 2017
Posts
9
Reaction score
16
climate finance.jpg

Miongoni mwa misemo maarufu mitaani ni pamoja na ule usemao “hakuna vya bure,” na kwa watumiaji wa lugha ya Kiingereza nao wanao usemao, “No free lunch.”

Hivi sasa, hii misemo ipo bayana kwa nchi masikini duniani na inajibainisha zaidi kwenye kile kinachoitwa misaada kwa ajili ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Nchi masikini duniani au kwa lugha nyingine huitwa zinazoendelea na kwa kifupi hufahamika zaidikwa lugha ya Kiingereza kama “Global South countries,” zinakamuliwa na mataifa tajiri (Global North) kupitia kampuni zao kubwa katika mnyorro unaojulikana kama “Corporate capture,” ambapo watu wachache wenye nguvu kubwa za kiuchumi na ambao kwa nguvu hiyo wanafifisha haki za binadamu na ustawi wa watu wengi.

Nguvu hizo hujidhihirisha zaidi kwenye umiliki wa njia kuu za uchumi na matumizi ya rasilimali/maliasili kunufaisha wachache.

Hali hiyo hujidhihirisha pia kwenye uharibifu wa mazingira ili kujinufaisha, uharibifu huu hatimaye hukandamiza haki za msingi za binadamu kama vile kupata chakula bora, maji salama, makazi bora na afya njema.

Mara nyingi, “corporate capture” ni mtandao wa kimataifa na unapenya hadi kwenye mashirika ya Umoja wa Mataifa, na ndio maana madhara yake huonekana takribani katika nchi zote masikini ambako matajiri wachache wanamiliki uchumi.

Taarifa ya utafiti kuhusu fedha kwa ajili ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi masikini na namna kampuni kubwa duniani zinavyofyonza pesa ya umma kupitia ruzuku za serikali katika nchi hizo inaonyesha kuchochea zaidi mitafaruku ya hali ya hewa.

Watafiti katika taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Kimataifa la ActionAid, wanatumia sekta za mafuta na kilimo kikubwa cha biashara (industrial agriculture), kuonyesha ukubwa wa tatizo wakisema mbali ya kuchangia uchafuzi wa hali ya hewa duniani, kampuni hizo pia huvuna zaidi ya shilling za Kitanzania trilioni 1.8 kila mwaka kutoka nchi masikini kupitia ruzuku ya serikali.

Kiwango hicho ni sehemu tu ya fedha inayofyonzwa na kampuni hizo kupitia ruzuku inayotolewa na serikali za nchi hizi masikini katika kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi na ni pesa ambayo ilitosha kugharamia elimu ya watoto wote kwenye nchi hizo masikini, tena ikiwa ni mara zaidi ya 3.5 ya gharama yao ya elimu.

Katibu Mkuu wa ActionAid, Arthur Larok anaielezea taarifa hiyo akisema,

“Taarifa hii inafichua tabia ya kinyonyaji kampuni tajiri duniani, wanaua maisha kwenye nchi masikini kwa kunyonya fedha za umma na kuchochea mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi.”

Ni wazi kwamba sehemu kubwa ya matumizi ya fedha ya umma kwenye nchi masikini (global south) huchotwa tena na kampuni zile zile, zinazohusika na uharibifu wa hali ya hewa unaoziumiza zaidi jamii katika nchi masikini.

Fedha hizo huzichota kupitia ruzuku ya serikali za nchi masikini inazotoa kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Baadhi ya kampuni za kimataifa zinazotajwa katika taarifa hiyo ya ActionAid, kunufaika kupitia ruzuku za nchi masikini, ni pamoja na Kampuni ya Mafuta ya Shell na kampuni kubwa ya kilimo duniani ijulikanayo kwa jina la Bayer, ambayo ni kampuni mama ya MONSATO.

Zambia ni mfano wa namna nchi masikini zinavyonyonywa na kampuni hizi kupitia ruzuku kwenye sekta ya kilimo, ambapo utafiti wa ActionAid unaonyesha kuwa asilimia 80 ya bajeti yake ya kilimo mwaka huu, imeelekezwa kwenye kilimo kikubwa, na zaidi ikiwa ni ruzuku kwenye mbolea na mbegu za viwandani na madawa, vyote vikichangia uchafuzi wa hali ya hewa.

Ni asilimia sita tu ya bajeti hiyo ndiyo ilibainika kuelekezwa kwenye Mpango wa Maendeleo ya Kilimo na Uzalishaji kusaidia wakulima kutumia kilimo chenye kurutubisha udongo kwa njia za asili na kupunguza utegemezi wa pembejeo za viwandani kama vile mbolea, mbegu na madawa.

Mnyororo huo unaonyesha kuwa utegemezi kwenye pembejeo za viwandani, huielekeza ruzuku yote hiyo kwenye ununuzi wa mbolea, madawa na mbegu kutoka kampuni kubwa duniani zinazozalisha bidhaa hizo.

Hii ni nchi moja tu, nchi nyingi masikini zipo katika mwelekeo huo huo, zikitengenezewa bomba la kupitisha fedha zao kwenda kunufaisha kampuni za mataifa tajiri duniani, hivyo kuziacha nchi masikini na watu wake kuongelea kwenye dimbwi la ufukara.

Mfumo wa uchumi wa aina hii, unazibana nchi masikini kwa kuzipitisha kwenye njia ambayo inadumaza maendeleo yao, huchochea uporaji ardhi, kuvuruga jamii zao, kuathiri usalama wa chakula, kuhatarisha haki za binadamu, kuharibu mfumo wa ikolojia na kuongezeka kukosekana haki katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Nchi hizi masikini zimejikuta katika mgogoro wa madeni unaokuzwa na kuongezeka kwa gharama za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuzilazimisha nchi nyingi masikini kuchukua uelekeo wa kutegemea nishati ya mafuta na kilimo kikubwa.

Nchi masikini zinalazimika kutafuta pesa za kigeni kwa ajli ya kulipia madeni wanayodaiwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), serikali na benki katika mataifa hayo tajiri duniani, hivyo kuruhusu sekta za mafuta na kilimo kikubwa kuimarisha nguvu zao juu ya uchumi wa nchihizo, na kisha pesa inayowekezwa kwenye sekta hizo huzirudisha kwao kupitia ruzuku inayowekwa na nchi masikini kwenye sekta hizo mbili.

Hivyo kuzuia nchi zilizo kwenye hatari ya kukabiliwa na mabadiliko ya tabianchi kufanya maamuzi sahihi ambayo yanaweza kusaidia kukabiliana na mgogoro wa tabianchi, mahitaji ya chakula na mahitaji ya nishati.

Ni wakati sasa kwa viongozi wa nchi masikini, kusimamia ustawi wa nchi zao, kwanza kuwa na sauti moja kwenye majukwaa ya kimataifa, hususani kwenye mikutano ya Umoja wa Matafa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP), hususani unaoanza mwezi ujao (COP29) pale Baku nchini Azerbaijan.

Miongoni mwa mambo wanayopaswa kuyasimamia ni pamoja na nchi tajiri kupunguza uzalishaji wa hewa chafu duniani katika kiwango kilichokubaliwa, kutekeleza ahadi za msaada wa fedha kwa nchi masikini kukabiliana na kuhimili madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi badala ya kujificha kwenye kivulicha mikopo ya nchi na benki zao.

Viongozi wa nchi masikini wanapaswa kutambua mtego wa madeni uliopo kupitia mikopo inayotolewa kwa madai ya fedha za kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi, kwani huzilazimisha nchi masikini kuishi kwa kutafuta fedha za kulipia madeni hayo badala ya kuendeleza na kuboresha huduma za kijamii zikiwemo sekta za afya, elimu na maji.
 
View attachment 3124481

Sawa wacha watoke vitambi!
 
Nguvu ya umaskini iko kwenye umoja wao.Matajiri kuanzia makampuni ya simu , bet n.k huungana kummaliza maskini.Ajabu maskini hawaungani kujitetea
Tamaa na ukafi wa viongozi nchi masikini ni jangaa
 
Back
Top Bottom