Uchaguzi 2020 Kampuni ya Afrika Kusini yashinda tenda kuchapisha karatasi za kura 2020

Uchaguzi 2020 Kampuni ya Afrika Kusini yashinda tenda kuchapisha karatasi za kura 2020

Mnaoshabikia zingechapishwa humu ndani hamjajaribu kuwaza kwamba zikichapishwa na printing press za humu...udanganyifu na duplications itakuwa wa hatari zaidi..bora kidogo zikitoka nje
kwamba zikichapishwa huko south ndio udanganyifu hautakuepo?
wangetaka udanganyifu usiwepo wasingeenda kuchapia karatasi south bali wangeweka tume huru ya uchaguzi
 
Gazeti la the Citizen lina ripoti kuwa kampuni ya Ms Ren-Form CC ndio imeshinda tenda ya bilioni 14.4 baada ya kuishinda kampuni ya kutoka Dubai.

Gazeti hilo linadai kuwa pia NEC hawajakubali au kupinga kampuni hii kushinda tenda hii na kuahidi kuwa watatoa taarifa ya kampuni na bei hivi karibuni.

Kampuni ya South Africa ilishinda tenda hii ambayo awali ilikuwa na gharama za bilioni 18 lakini NEC wakakaa mezani na kuishusha mpaka bilioni 14.4.

Mchakato wa kushusha bei ya tenda uliifanya kampuni ya Dubai, ambayo ndiyo ilichapa karatasi za uchaguzi wa Malawi 2020, kutuma malalamiko yake ambayo yalikataliwa na Ms Ren-form CC kushinda tenda hiyo.

Chanzo: South Africa firm to print Tanzania's 2020 ballot papers
Nchi ya viwanda tunashindwaje kutoa hiyo tenda kwa wazawa?

Kampuni ya Dubai kama ndio walichapisha za uchaguzi wa malawi, basi hatuna imani nayo kwa sababu inawezekana zikawa na gundu kwa chama tawala.

Na huko SA nina wasi wasi na hiyo kampuni iliyoshinda, isije ikawa yule mkulima ana hisa ndani yake.
 
Gazeti la the Citizen lina ripoti kuwa kampuni ya Ms Ren-Form CC ndio imeshinda tenda ya bilioni 14.4 baada ya kuishinda kampuni ya kutoka Dubai.

Gazeti hilo linadai kuwa pia NEC hawajakubali au kupinga kampuni hii kushinda tenda hii na kuahidi kuwa watatoa taarifa ya kampuni na bei hivi karibuni.

Kampuni ya South Africa ilishinda tenda hii ambayo awali ilikuwa na gharama za bilioni 18 lakini NEC wakakaa mezani na kuishusha mpaka bilioni 14.4.

Mchakato wa kushusha bei ya tenda uliifanya kampuni ya Dubai, ambayo ndiyo ilichapa karatasi za uchaguzi wa Malawi 2020, kutuma malalamiko yake ambayo yalikataliwa na Ms Ren-form CC kushinda tenda hiyo.

Chanzo: South Africa firm to print Tanzania's 2020 ballot papers
Kiwanda gani kitafanya yafuatayo ili pesa ibaki nyumbani?

1.Kuchapisha karatasi za kupiga kura(ballot paper)
2.Kuchapisha daftari la wapiga kura
3.Kutengeneza mabox ya kukusanya kura
4.Kutengeza box-chumba cha kupigia kura
5.Kutengeneza t-shirt na kofia za tume ya uchaguzi

Bendera,na sare mbalimbali za vyama vya siasa vyote hivi najiuliza ndani ya hii miaka 5 ya serikali ya viwanda kuna hatua yoyote ya kuzuia hizi hela zisiende nje ya nchi?

Je 2025 bado mtindo ni huuhuu?

Kitu gani kinazuia uwekezaji kwenye viwanda?
Magufuli viwanda viko wapi ?
 
Back
Top Bottom