Uchaguzi 2020 Kampuni ya Afrika Kusini yashinda tenda kuchapisha karatasi za kura 2020

Mnaoshabikia zingechapishwa humu ndani hamjajaribu kuwaza kwamba zikichapishwa na printing press za humu...udanganyifu na duplications itakuwa wa hatari zaidi..bora kidogo zikitoka nje
kwamba zikichapishwa huko south ndio udanganyifu hautakuepo?
wangetaka udanganyifu usiwepo wasingeenda kuchapia karatasi south bali wangeweka tume huru ya uchaguzi
 
Nchi ya viwanda tunashindwaje kutoa hiyo tenda kwa wazawa?

Kampuni ya Dubai kama ndio walichapisha za uchaguzi wa malawi, basi hatuna imani nayo kwa sababu inawezekana zikawa na gundu kwa chama tawala.

Na huko SA nina wasi wasi na hiyo kampuni iliyoshinda, isije ikawa yule mkulima ana hisa ndani yake.
 
Kiwanda gani kitafanya yafuatayo ili pesa ibaki nyumbani?

1.Kuchapisha karatasi za kupiga kura(ballot paper)
2.Kuchapisha daftari la wapiga kura
3.Kutengeneza mabox ya kukusanya kura
4.Kutengeza box-chumba cha kupigia kura
5.Kutengeneza t-shirt na kofia za tume ya uchaguzi

Bendera,na sare mbalimbali za vyama vya siasa vyote hivi najiuliza ndani ya hii miaka 5 ya serikali ya viwanda kuna hatua yoyote ya kuzuia hizi hela zisiende nje ya nchi?

Je 2025 bado mtindo ni huuhuu?

Kitu gani kinazuia uwekezaji kwenye viwanda?
Magufuli viwanda viko wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…